Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limeelezea
masikitiko makubwa kufuatia kifo cha golikipa na nahodha wa timu ya
Taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana).
Senzo Meyiwa (27) ambaye alikuwa golikipa na nahodha wa timu ya Orlando Pirates alipigwa risasi na majambazi siku moja baada ya kuiongoza timu yake kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Ajax Cape Town kwenye robo fainali ya kombe la Ligi.
Katika salamu zake kwa Chama cha Mpira cha Afrika Kusini (SAFA, TFF imesema kifo cha ghafla cha nahodha huyo wa Bafana Bafana ni pigo kubwa kwa familia yake, klabu yake ya Orlando Pirates, familia ya mpira na taifa zima la Afrika Kusini.
“ Shirikisho la Mpira Tanzania na familia ya mpira kwa ujumla iko nanyi katika hiki cha maombolezo”. Ilisema sehemu ya salamu hizo iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine.
“Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pa amani ya milele”. Amen.
Nakala ya salamu hizo imetumwa kwa Mwenyekiti wa ligi kuu ya Afrika Kusini (PSL) na Mwenyekiti wa klabu ya Orlando Pirates.

No comments:
Post a Comment