Ujanja ya maboresho ya kikosi uliodhamiriwa kufanywa na
meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger umebainika baada ya vyombo vya
habari kuwekwa hadharani mpango wa kutaka kumsajili beki wa kati wa
klabu ya West Ham Utd, Winston Reid.
Wenger, ametajwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili beki huyo kutoka nchini New Zealand kwa kutumia kigezo cha mkataba wake kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.
Mipango yam zee huyo kutoka nchini Ufaransa, ni kumsajili Reid itakapofika mwezi januari mwaka 2015 ambapo anaamini ada yake ya usajili itakuwa hafifu.
Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, la nchini Uingereza imeelezwa kwamba bosi huyo wa The Gunners, amekua akimfuatilia Reid mwenye umri wa miaka 26 kwa kipindi kirefu na taarifa za mkataba wake kuwa mbioni kufikia kikomo zimemfurahisha.
Hata hivyo mbali na klabu ya Arsenal kutajwa katika mikakati ya kutaka kumsajili Reid klabu kadhaa za nchini Uingereza nazo zina mikakati ya kutaka kumsajili.
Reid, kwa sasa ndio nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya New Zealand na tangu alipojiunga na klabu ya West Ham Utd mwaka 2010 amecheza michezo 102 na kufunga mabao 6.

No comments:
Post a Comment