Kijana aliyejiunga na IS atoa onyo - LEKULE

Breaking

23 Oct 2014

Kijana aliyejiunga na IS atoa onyo

Kijana mmoja raia wa Australia, aliyejiunga na kundi la wapiganaji wa IS wanaopigana nchini Iraq na Syria ameonekana kwenye kanda ya video.
Katika kanda hiyo kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 anawahutubia waziri mkuu wa Australia Tony Abbot pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama.
Kijana huyo kwa jina Abdullah Elmir ambaye pia anajiita,Abu Khaled, alisema "hatutasalimisha silaha zetu hadi tutakapofika katika ardhi yenu. ''
Alitoroka kutoka nyumbani Australia mwezi Juni na kijana mwingine raia wa Australia na inaaminika alisafiri kwenda Syria kupitia Uturuki.
Msemaji wa serikali amesema kanda hiyo ni idhara ya tishop la kundi la Islam ic State kwa dunia nzima.
''Na hiyo ndio maana Australia imejiunga na muungani wa wanjeshi wanaopigana dhidi ya ISIL nchini Iraq,'' alisema msemaji huyo.
Australia inachangia pakubwa majeshi katika muungano wa majeshi wa Unaoongozwa na Marekani ambalo linadhibiti baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq.
Muungano huo una kikosi cha wanajeshi 600.
Mapema wiki hii muungano huo ulikubaliana na Iraq kuipa wanajeshi 200 wenye ujuzi wa hali ya juu kutoa mafunzo kwa wanajeshi ili kupigana na wapiganaji wa IS.
Pia walitangaza tisho la mashambulizi kuwa juu mwezi Septemba huku kukiwa na wasiwasi kuhusu wapiganaji wanaorejea kujiunga na wapiganaji hao wa kiisilamu baada ya taarifa za kijasusi kuonyesha kuwa wapiganji hao wanapanga kufanya mashambulizi.
Katika kanda fupi ya video iliyowekwa kwenye mtandao, Abdullah Elmir waliwahutubia viongozi hao kwa kusema:''Kwa viongozi, kwa Obama,kwa Tony Abbott nasema hivi, hizi silaha tulizo nazo , wanjeshi hawa hatutakoma kupigana, hatutasalimisha silaha zetu hadi tutakapofika katika ardhi yenu. ''
"Hadi tutakapoweka bendera nyeusi katika kasri ya Buckingham Palace, una hadi tutakapoweka bendera yetu katika Ikulu ya Marekani, hatutasitisha vita,'' alisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 17.

No comments: