TUME YA MABADILIKO YA KATIBA YAVUNJWA RASIMU. - LEKULE

Breaking

25 Mar 2014

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA YAVUNJWA RASIMU.


TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME
YA MABAADILIKO YA KATIBA.

Mhe.Raisi aliunda tume ya mabadiliko ya katiba kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha sheria ya mabadiliko ya katiba,sura ya 83 kwa tangazo la serikali na.110 la mwaka 2012.Tume ilikusanya maoni na kuandaa rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye bunge maalumu.

Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha sheria ya mabadiliko ya katiba,sura ya 3,Raisi amepewa mamlaka ya kuvunja tume ya mabadiliko ya katiba baada ya rasimu ya katiba kuwasilishwa bungeni.

Mnamo tarehe 18 march,2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji JOSEPH SINDE WARIOBA aliwasilisha rasimu ya katiba kwenye bunge maalum.Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha sheria ya mabadiliko ya katiba.Raisi wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi TUME YA MABADILIKO YA KATIBA tarehe 19 march,2014 kwa tangazo la serikali na.81 la tarehe 21 march 2014.Hivyo kwa tangazo hilo,shughuli zote za Tume ya mabadiliko ya katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 march 2014.


Imetolewa na

kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi Ikulu
DAR ES SALAAM.

No comments: