MICHANGO YA WABUNGE KATIKA REPORT YA OPERATION TOKOMEZA UJANGILI. - LEKULE

Breaking

22 Dec 2013

MICHANGO YA WABUNGE KATIKA REPORT YA OPERATION TOKOMEZA UJANGILI.

ZITTO KABWE; Waziri mkuu fanya uwajibikaji wa kisiasa na siyo kwamba kwa kufanya hivyo unahusika la hasha.....kama huchukui hatua Bunge libebe dhamana hiyo. KANGI LUGOLA; Makosa ya Operation hiyo yalianza mapema wakati operation ya kijeshi ilipopelekwa kwa raia. MCHUNGAJI PETER MSIGWA. Kama mnatuheshimu,mheshimiwa waziri mkuu ungekuwa unatayarisha makaratasi saa hizi unaandika barua ya kujiuzulu. LEKULE LAIZER; Bunge livunjwe endapo waziri mkuu na mawaziri hao wanne watakataa kujiuzulu. ANNA KILANGO MALECELA; Serikali yangu ya CCMlazima ichukue hatua leo tusisubiri kesho,kwani matatizo yaliyotokea ni makubwa sana,uamuzi uchukuliwe leo leo hii. MH.JAMES MBATIA Bungeni kazi yetu,sisi wabunge ni kuisimamia serikali kwa hiyo wale wabunge waliotajwa kwenye ripoti watajwe ili nao wawajibike ili bunge letu liwe na nia thabiti ya kuisimamia serikali.

No comments: