Wazanzibari Watakiwa Kuhakiki Simu Zao Haraka Ili Kupeka Kufungiwa Ifikapo Mwezi Wa Saba - LEKULE

Breaking

4 Feb 2016

Wazanzibari Watakiwa Kuhakiki Simu Zao Haraka Ili Kupeka Kufungiwa Ifikapo Mwezi Wa Saba



Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka Wazanzibari kuhakiki simu zao za mkononi ili kuepuka kufungiwa mawasiliano ifikapo Julai, mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya kuwapo ambazo ni feki.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja jana, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema ni vyema wananchi wote kuhakiki simu zao ili wakati wa kufungia zisizofaa wasikose mawasiliano.

Mungy alisema TCRA imefikia uamuzi wa kutekeleza matakwa ya sheria kutokana na kuwapo kwa vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa maadili kwa kutumia simu.

Alisema kumekuwapo na utumiaji wa simu usio mzuri unaofanywa na baadhi ya wananchi, ikiwamo baadhi yao kuzisajili kwa kutumia majina ya watu ili kuepuka kutambulika wanaposhiriki uhalifu.

“Pamoja na kuwapo kwa baadhi ya watu kusajili simu kwa maji na yasio yao, lakini pia kumekuwapo na vitendo vya wizi wa simu. Hivyo tunaamini wazi kuwa njia hii kwa kiasi kikubwa itasaidia jamii, kwani hata mtu akiiba simu kwa mujibu wa taratibu zetu hataweza kuitumia,”alisema.

Meneja huyo alisema mfumo unaotarajiwa kutumika nchi nzima utamlazimisha mtumiaji wa simu kutumia inayokubalika kisheria, huku usajili wake ukiwa hauna mashaka.

Alizitaja baadhi ya njia ambazo mtumiaji wa simu atahitajika kuzizingatia kabla na baada ya kununua kuwa ni kuhakikisha inalingana na mabadiliko ya kiteknolojia na kupewa muda maalumu wa kutumia usiopungua miezi 12.

Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Matumizi ya Mitandao wa TCRA, Thoday Ringo alisisitiza haja ya wananchi kuwa makini kununua simu zenye ubora.

Alisema baadhi ya watu wamekuwa wepesi kununua simu zinazouzwa kwa bei ya chini bila ya kujua madhara yake.

“Napenda kuwatahadharisha ndugu zangu kuepuka kununua simu ovyo, la msingi ujue kuwa zipo ambazo ni feki,” alisema. 
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya TCRA Innocent Mungy, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari baada ya kuangalia simu zao baada ya kuingiza namba hizo na kugunduwa kuwa ziko salama na siyo feki. kwa bahati nzuri takribani waandishi wote simu zao zilikuwa  orijino.

No comments: