Magufuli Ataka Bandari Zilindwe Na Jeshi La Polisi Kama Ilivyokuwa Hapo AwaliRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini kurejesha kitengo cha ulinzi bandarini na pia eneo ambalo linafungwa mita za mafuta.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imesema Rais Magufuli ametaka jeshi la polisi nchini kurejesha ulinzi kama ilivyokuwa nyakati za nyuma kabla mamlaka ya bandari haijaamua kubandilisha mfumo wa kuweka walinzi wake.

Balozi Ombeni Sefue ameongeza kuwa katika eneo ambalo linafungwa mita za mafuta (Flowmeters), ambalo waziri mkuu alitembelea na kumsimamisha mkurugenzi wa wakala wa vipimo sasa ni lazima lilindwe na jeshi la polisi.
Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Powered by Blogger.