Museveni: Nimeandaa Mrithi wa Mashamba Yangu Lakini Sio Mrithi wa Uganda.....Hakuna Chama Cha Kutuondoa Madarakani - LEKULE BLOG

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 16 February 2016

Museveni: Nimeandaa Mrithi wa Mashamba Yangu Lakini Sio Mrithi wa Uganda.....Hakuna Chama Cha Kutuondoa Madarakani


Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba ameandaa mrithi wa shamba lake lakini sio mrithi wa Uganda na Waganda watachagua mtu wa kuwaongoza pale ambapo yeye atastaafu wadhifa huo.

Museveni ameyasema hayo kipindi ambapo kampeni za lala salama zinaendelea nchini Uganda na uchaguzi wa kumpata Rais wa nchi hiyo unafanyika siku ya Alhamisi ya wiki hii.

Rais Museveni ambaye amedumu madarakani kwa muda wa miaka 30 anatetea tena nafasi yake hiyo huku akitamba kuwa hakuna chama chenye uwezo wa kuweza kushinda chama chake cha National Resistance Movement (NRM)

“Sidhani vyama vya upinzani vitashinda NRM. Kwa sababu tunajua nguvu yetu. Tunajua tutashinda, lakini kama itakuwa tumeshindwa basi tutawaachia wale ambao wameshinda. Lakini sidhani kuna chama kinaweza kushinda NRM wakati huu,” amesema

Aidha kwa sasa katiba inaeleza umri wa juu zaidi wa Rais kuwa madarakani ni miaka 75. Kwa sasa Rais Museveni anakaribia kutimiza umri wa miaka 72 ikimaanisha kwamba katika mwaka wake wa mwisho wa muhula ujao iwapo ataingia madarakani, atakuwa na umri wa miaka 76.

Chanzo BBC
Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages