Mashabiki wa soka Ujerumani wamempigia kura Ozil na kushinda tuzo hii kwa mara ya nne - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 15 January 2016

Mashabiki wa soka Ujerumani wamempigia kura Ozil na kushinda tuzo hii kwa mara ya nne

January 14 tovuti ya timu ya taifa ya Ujerumani imetangaza jina la mchezaji bora wa kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kwa mwaka 2015, tovuti hiyo imetangaza jina hilo la mchezaji bora wa mwaka 2015 baada ya mashabiki 51000 kupiga kura na asilimia 45.9 ya kura hizo kumuangukia Mesut Ozil.
Mesut Ozil ameongoza kwa kupata asilimia nyingi ya kura hizo, huku akifuatiwa na mshambuliaji wa FC Bayern Munich Thomas Muller ambaye alikuwa na kura asilimia 15.9, Mesut Ozil kwa mwaka 2015 aliichezea Ujerumani jumla ya mechi nane kati ya tisa ilizocheza Ujerumani. Katika mechi hizo nane Ozil amekimbia jumla ya Kilometa 92.71 ambazo ni wastani wa Kilometa 11.59 kwa dakika 90 za mchezo.
csm_81736-OEzil_Georgien2_f0c9bcaa09
Kwa mwaka 2015 Mesut Ozil amepiga jumla ya mashuti 14 akiwa na Ujerumani na ana assist 6 katika michezo nane, hii ni mara ya nne kwa Ozil kutwaa tuzo hiyo. Ozil aliwahi kutwaa tuzo hiyo mwaka 2011, 2012, 2013 na 2015.
Post a Comment