Kalapina afungukia kumsifia Rais Magufuli - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Tuesday, 5 January 2016

Kalapina afungukia kumsifia Rais Magufuli


MKALI wa nyimbo za harakati na aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupita tiketi ya Chama cha ACT, Kalama Masoud, ‘Kala Pina’ amefungukia sababu za kumsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kupitia wimbo wake wa Magufuli Balaa.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Kala Pina alisema kuwa japo kuwa yeye anatokea chama cha upinzani lakini hiyo haimaanishi kuwa lazima apinge kila kitu na kudai kuwa amependa kasi ya utendaji wa rais na yeye kama msanii ameona ni vyema kutoa wimbo huo ili kuelezea hisia zake.

“Mimi ni mwanaharakati na harakati siyo upinzani ni kujenga nchi, rais amenifurahisha nami kama msanii nimeamua kumtungia wimbo ili kuelezea hisia zangu kwake siyo eti kwa kuwa mimi ni mpinzani nipinge tu,” alisema Kala Pina.
Post a Comment