GOLI LA KISIGINO LA ROONEY LAWEKA REKODI TATU TOFAUTI - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 3 January 2016

GOLI LA KISIGINO LA ROONEY LAWEKA REKODI TATU TOFAUTI

Rooney-waza
Goli la kisigino alilofunga mshambuliaji na nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney jana katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England dhidi ya Swansea City, halikutosha kuipa ushindi tu timu yake na kuipa points 3 pekee, bali pia lilimfanya mshambuliaji huyo kushika nafasi ya pili nyuma ya mkongwe Alan Shearer katika upachikaji wa mabao wa muda wote katika historia ya ligi hiyo.
Alan Shearer ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote hadi sasa ana magoli 260 huku Wayne Rooney akifikisha magoli 188 siku ya jana na kuwa nyuma yake kwa tofauti ya magoli 72.
Goli hilo pia ambalo ni la kwanza kwa Rooney tangu alipofunga mwezi wa kumi mwaka jana limemfanya pia nahodha huyo wa timu ya taifa ya England pia kupunguza tofauti kati yake na kinara wa mabao katika historia ya klabu ya Manchester United, Sir Bob Chalton ambapo Wayne Rooney amebakiza goli 11 tu kumfikia mkongwe huyo na kuweka rekodi yake mpya ya kuwa kinara wa mabao wa muda wote.
Tayari mshambuliaji huyo amekwisha weka rekodi ya ufungaji na kuwa mfungaji bora wa muda wa muda wote katika timu ya taifa ya England kwa kuvunja rekodi iliyokua imesimama kwa muda mrefu ya Sir Bob Chalton ambaye alifunga mara 49 kabla ya Rooney kufunga magoli 50.

Rooney sasa ana miaka 30 na inasubiriwa kuona kama anaweza kufunga magoli 11 ili awe kinara wa magoli katika klabu yake ama goli 72 ili kutengua rekodi ya Alan Shearer ya ufungaji katika historia ya ligi kuu nchini humo.
Post a Comment