Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed
Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana akifuatana na
Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa
madawati 100 kwa ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo
utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar
Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa
Uongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu
Mjini Zanzibar jana kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)
ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa
pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mashekhe wa Jumuiya ya
Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh Maulana
Dhishan Haidar na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza (kushoto)
wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa madawati 100
kawanafunzi wa Zanzibar,
Rais wa
Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Raza (kushoto) akitoa maelezo kwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (kulia aliyekaa) wakati Jumuiya hiyo ilipofika Ikulu Mjini
Zanzibar jana kukabidhi madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar
ikiwa ni katika katua za kuimarisha sekta ya Elimu nchini.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa
pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya ya
Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed Raza
walipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana,msaada huo kwa ajili ya wanafunzi
wa Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesema kuwa nia na malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
kuimarisha sekta ya elimu ni makubwa hivyo kujitokeza kwa wanannchi na
taasisi mbali mbali kuiunga mkono sekta hiyo ili izidi kuimarika ni
jambo la faraja.
Dk. Shein
aliyasema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na viongozi na Masheikh
wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakiongoza na Rais wa Jumuiya hiyo
Mohammed Raza waliofika Ikulu mjini Zanzibar kumkabizi Rais msaada wa
madawadi yaliotolewa na uongozi huo pamoja na familia ya Rais wa Jumuiya
hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar.
Katika
maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inathamini na imekuwa ikichukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha
sekta ya elimu inaimarika na ndio maana Rais wa Kwanza wa Zanzibar mara
baada ya ukombozi alitangaza elimu bure.
Dk. Shein
alisema kuwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Zanzibar ina
historia kubwa ya elimu ya dini na dunia kwani ndio nchi iliyokuwa ya
mwanzo kuwa na elimu ya dini mnamo miaka 1890 na elimu ya dunia kuanzia
mwaka 1905 kwa kuanzisha skuli licha ya kuwa elimu hiyo ya dunia
waliipata watu wachache.
“Tumefarajika
sana, tunajiona hatupo peke yetu tupo na wenzetu katika kulitafutia
ufumbuzi suala hili, madawati ni muhimu kwa ajili ya wanafunzi
wetu…..ipo siku Zanzibar itakuwa haina shida ya madawati” alisema Dk.
Shein.
Aidha,
Dk. Shein alieleza kufarajika kwake na mwanzo mzuri uliooneshwa na
Jumuiya hiyo pamoja na familia ya Mohamed Raza kwa kutoa mchango wa
madawati hayo ambayo yatasaidia katika kuimarisha sekta ya elimu hapa
nchini kwa kuwasaidia wanafunzi kupata vikalio vya uhakika maskulini.
Mapema
Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Zanzibar, Mohammed Raza
alimueleza Dk. Shein kuwa Jumuiya yake imetoa msaada wa madawati 50 na
mtoto wake Hassan Mohammed Raza ametoa madawati 50 yenye thamani ya Tsh.
milioni 12 kwa ajili ya wanafunzi wa skuli za Zanzibar huku akiahdi
kuwa misaada hiyo itakuwa endelevu.
Katika
maelezo yake Raza alisema kuwa msaada huo una lengo la kuunga mkono azma
ya Dk. Shein ya kuhakikisha suala la upatikanaji wa madawati linapatiwa
ufumbuzi hapa nchini hali ambayo ilimpelekea Rais kuunda Kamati ya
Kitaifa ya watu 12 ikiongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia
ni Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman.
Rais huyo
wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo
la Uzini alisema kuwa Jumuiya yake itaendelea kutoa misaada katika
sekta zote za maendejana ikiwemo elimu, afya na nyenginezo huku akiahidi
kuwa atahakikisha kwa kushirikiana na Waziri wa Elimu anachukua juhudi
kusafiri hadi nje ya Zanzibar kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi suala
hilo.
Nao
Masheikh kutoka Jumuiya hiyo wakiongozwa na Sheikh Maulana Dhishan
Haidar walitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Dk. Shein kwa uongozi wake
mahiri sambamba na juhudi zake za kuendelea kusimamia amani na utulivu
hapa Zanzibar.
Viongozi
hao walieleza azma yao ya kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar pamoja na kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Shein katika
kuimarisha sekta mbali mbali hapa nchini.
“Zanzibar
imeweza kupata maendejana…watu wake wanapendana….amani na utulivu
umeimarika kwa kiasi kikubwa haya yote yanatokana na uongozi bora wa Dk.
Shein”,alisema Maulana Haidar.
Nae
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma alitoa pongezi na
shukurani kwa Jumuiya na Familia ya Mohammed Raza kwa kutoa msaada huo
wa madawati ambayo yatawasaidia wanafunzi wa hapa Zanzibar katika kuweza
kujipatia elimu bora kwa ufanisi zaidi.
Waziri
Pembe alisema kuwa Wizara kwa upande wake inatoa shukurani kubwa na
inathamini mchango huo na kueleza kuwa kwa vile Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ina nia nzuri juu ya jambo hilo anamatumaini makubwa kuwa
mafanikio yatapatikana.
Waziri
huyo wa Elimu alitumia fursa hiyo kupongeza juhudi zinazochukuliwa na
Dk. Shein katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendejana ikiwemo
sekta ya elimu na kuwaomba wananchi na taasisi nyengine kuendelea kutoa
michango yao ya vifaa hivyo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar.
Hivi
karibuni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwasilisha rasimu ya
uchangiaji na upatikanaji wa madawati maskulini ili kuweza kupunguza
upatikanaji wa madawati katika skuli za Zanzibar katika Baraza la
Wawakilishi.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
No comments:
Post a Comment