Shirika
la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF, limeonya kwamba
watoto walio na umri chini ya miaka 5 watafariki kutokana na sababu
zinazoweza kuzuilika kati ya sasa na mwaka 2030.
Katika
ripoti yake ya mwaka UNICEF imesema kwamba kulingana na mwenendo wa hivi
karibuni na makadirio ya ukuaji wa watu, watoto milioni 167 wataishi
katika umaskini uliokithiri, milioni 60 hawataweza kuhudhuria elimu ya
msingi na wanawake milioni 750 watakuwa katika ndoa kama watoto ifikapo
mwaka 2030, labda ikiwa suala la usawa litashughulikiwa na nchi
ziharakishe jitihada za kuboresha afya na elimu kwa wasiojiweza.
Naibu
mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Justin Forsyth amesema katika uzinduzi wa
ripoti hiyo na "kutuma ujumbe kwa dunia isiyo salama" hasa wahamiaji na
wakimbizi ikiwa ni pamoja na mamilioni ya watoto.
Sababu zinazochangia
Wengi
wanakimbia kwa sababu ya umaskini na kukosekana kwa usawa, amesema
mkurugenzi huyo na kwamba sababu hizo zinaweza kushughulikiwa.
"Kazi
yetu kama UNICEF ni kuwepo na kusaidia watoto kuishi" alisema Forsyth,
akiongeza kwamba shirika hilo linapaswa kuhakikisha kunakuwa na mjadala
mzito wa kuhusu masuala magumu na kupaza ujumbe wa kuwasaidia
wasiojiweza.
Mkurugenzi
wa programu UNICEF Ted Chaiban amesema katika nyongeza ya vijana
wanaokimbia umaskini na kukosekana kwa usawa, pia wapo watoto zaidi
wanaoishi katika maeneo ya vita karibu milioni 250 na wengine milioni 30
hawana makazi..
Kwa
mujibu wake, ukosefu wa usawa upo kila nchi na watoto asilimia 20
duniani maskini ya wakazi ni mara mbili ambao watafariki katika umri
chini ya miaka mitano zaidi ya asilimia 20 ya watoto tajiri.
Hali ni mbaya
Ripoti
hiyo inasema asilimia 80 ya vifo vinavyoweza zuilika vinatokea katika
maeneo ya kusini mwa Asia na kusini mwa jangwa la Sahara, nusu ya hivyo
ni katika nchi za India, Nigeria, Pakistan, Congo na Ethiopia.
UNICEF
imewataka nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa kubuni mipango ya
kitaifa ikayowasaidia wasiojiweza na watoto walioachwa kando kwanza
pamoja na kujiwekea malengo maalumu ya kupunguza pengo kati ya maskini
na tajiri.
Ripoti
hiyo inaona kwamba karibu watoto milioni 147 walio na umri wa mwaka
mmoja hadi mitano wanaweza kuokolewa kutokana vifo kwa kuongeza matumizi
ya asilimia 2 tu katika nchi 74.
UNICEF
imesema pia kwamba ina ushahidi wa kila dola moja inayotumika katika
chanjo kwa watoto wasiojiweza inaweza kuzalisha dola 16 katika suala la
faida za kiuchumi.
Kulingana
na " Ripoti ya Hali ya Watoto Duniani 2016, " fedha za uhamisho
zimesaidia watoto kukaa katika shule kwa muda mrefu na kwa wastani, kila
mwaka wa elimu , mtoto anapata ongezeko la mapato ya mtu mzima kwa
asilimia 10 .DW
No comments:
Post a Comment