Washambuliaji
wa kujitowa muhanga wamewauwa zaidi ya watu 41 na kujeruhi wengine 140
katika shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa Ataturk mjini Istanbul
katika mfululizo wa miripuko ya mabomu dhidi ya Uturuki.
Idadi ya
watu waliouwawa katika shambulio la uwanja wa ndege wa Istanbul
imeongezeka na kufikia 41. Awali Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yidirm
amesema watu 36 wameuwawa hapo jana wakiwemo washambuliaji watatu wa
kujitowa muhanga ambao waliwasili katika uwanja wa ndege huo kwa kutumia
taxi na kujiripuwa mara tu baada ya kuanza kufyatuwa risasi.Waziri wa
sheria wa Uturuki Bekir Bozdag amesema watu 147 wamejeruhiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege huo baada ya kutokea kwa
shambulio hilo hapo jana Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yidrim amesema
kundi la Dola la Kiislamu linaonekana kuhusika na shambulio hiilo
Binali
amesema "Uchunguzi wa vikosi vyetu vya usalama unaashiria kwamba
shambulio hilo la kigaidi limetekelezwa na kundi la Daesh na licha ya
kwamba uchunguzi unakielekezea kidole kundi hilo la Dola la Kiislamu
uchunguzi huo bado unaendelea.Uwanja wa ndege unafunguliwa tena kwa
safari saa nane usiku na safari za ndege zitarudi katika hali ya
kawaida."
Kwa
mujibu wa maafisa polisi ilifyatuwa risasi kujaribu kuwazuwiya
washambuliaji wawili kabla hawajafika kituo cha ukaguzi wa usalama
katika ukumbi wa kuwasili abiria katika uwanja wa ndege huo lakini
waliripuwa mabomu yao. Afisa wa Uturuki amesema wengi waliouwawa
walikuwa ni raia wa Uturuki lakini pia kuna wageni miongoni mwa watu
waliouwawa.
Shambulio lafanana na la Brussels
Shambulio
hilo kwa kiasi fulani linafanana na shambulio la kujitowa muhanga
lililofanywa na wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu katika uwanja wa
ndege wa Brussels hapo mwezi wa Machi na kuuwa watu 16 kabla ya
shambulio jengine kuuwa watu wengine 16 siku hiyo hiyo katika njia ya
reli ya chini ya ardhi katika mji mkuu huo wa Ubelgiji.
Mashahidi
walirepoti kusikia milio ya risasi kutoka sehemu mbali za uwanja wa
ndege huo wa Atartuk ambao ndio uwanja wa ndege mkubwa kabisa nchini
Uturuki na wa tatu kwa kuwa na harakati kubwa za safari za kimataifa
barani Ulaya.
Rais Recep Tayyip Erdogan amelani shambulio hilo la kigaidi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.
Uwanja wafunguliwa tena
Ndege
tayari zimeanza kutuwa tena katika uwanja wa ndege huo leo ajafiri baada
ya uwanja wa ndege huo kufungwa kabisa kwa masaa kadhaa hapo jana
kufuatia shambulio hilo la kigaidi.Mamia ya safari zilifutwa kufuatia
shambulio hilo.
Shirika
la ndege la Uturuki ambalo limefuta zaidi ya safari 340 limekuwa
likiwarejeshea abiria fedha zao au tiketi mbadala lakini bado kuna
mkanganyiko kwa wasafiri wengi.
Shambulio
hilo la jana ni baya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa zaidi ya
muongo mmoja mjini Istanbul.Kundi la Dola la Kiislamu limekuwa
likilaumiwa kwa kuhusika na mashambulio kadhaa nchini Uturuki katika
kipindi cha mwaka mmoja uliopita.DW
No comments:
Post a Comment