Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi
Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mkutano wa 49 wa Kamisheni ya
Umoja wa Mataifa Kuhusu Idadi ya watu na Maendeleo. Pamoja na Mambo
mengine, Balozi anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo
amesema, ili ufuatiliaji wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo
endelevu panahitajika taarifa sahihi za takwimu.Sehemu ya wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Kimesheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya watu na Maendeleo.
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema takwimu sahihi zitahitajika katika kufuatilia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu maarufu kama Agenda 2030.
Hayo yameelezwa siku ya jumatano na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, wakati wa Mkutano wa 49 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya Watu na Maendeleo ( CPD), mkutano unaoendelea hapa Umoja wa Mataifa.
Balozi Manongi anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, amesema, hapana shaka kwamba ili nchi iwe na takwimu sahihi, zenye viwango vinavyokubaliwa kitaifa na kimataifa panahitajika ushirikiano baina ya Idara za Kitaifa za Takwimu, Serikali na washirika wa maendeleo.
“Upatikanaji wa takwimu zenye viwango katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu unatutaka tuwe wabunifu na tuboreshe mifumo yetu ya takwimu. Na katika hili, tusijidanganye, haya yote yanahitaji uwekezaji wa raslimali fedha na utaalam, patahitajika ushirikiano ambao utasaidia kuimarisha takwimu na kusaidia utekelezaji wa Agenda 2030”. Akaeleza Balozi Manongi.
Vilevile Mwakilishi huyo wa Tanzania, akaongeza kuwa takwimu sahihi zina uwezo wa kuleta tofauti mkubwa kwa vile zinawasaidia watendaji wa serikali katika upangaji wa sera na zinatoa ushahidi wa wapi palipofanikiwa na wapi pana matatizo au mapungufu.Na akasisitiza kwa kusema “ Takwimu sahihi zinasaidia uwazi na kubwa zaidi uwajibikaji”.
Akizungumzia Zaidi nafasi ya takwimu sahihi na zenye viwango, Balozi Manongi amesema, Tanzania inapenda kusisitiza tena umuhimu wa ukusanyaji wa takwimu kuhusu idadi ya watu kwa kile anachosema ni nguzo muhimu katika siyo tu ufuatiliaji wa utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya watu na Maendeleo lakini pia utekelezaji wa Ajenda 2030.
Akifafanua Zaidi kuhusu idadi ya watu, Balozi amesema, Tanzania ni kati ya nchi zenye ongezeko kubwa la idadi ya watu na hususaji vijana wanaoingia katika soko la ajira.“Ongezeko la vijana lina fursa na changamoto pia. Tunatambua kwamba ili nchi yetu inufaike na uwepo wa idadi kubwa ya vijana tunahitaji kuwa na mipango na sera madhubuti, ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo na stadi ambazo zitaiwezesha serikali kuvuna utaalamu na ujuzi wao” akabainisha Balozi.
Pamoja na ongezeko la idadi kubwa ya vijana, Balozi Manongi amesema kuna ongezeko pia la wazee wa miaka 60 na kuendelea hali inayoongeza mahitaji ya huduma za jamii na hususani afya. “ Ndiyo maana tunatambua muingiliano wa idadi ya watu na maendeleo”.
Pamoja na kuzungumzia changamoto mbalimbali za ukusanyaji wa takwimu sahihi na zenye ubora, Balozi amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, Serikali ya Tanzania imeendelea na juhudi za kuiwezesha Idara ya Taifa ya Takwimu, ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kisheria kuwa chombo pekee chenye mamlaka ya utoaji na usambazaji wa taarifa zinazohusiana na masuala ya takwimu.
Akatumia nafasi hiyo kutambua siyo tu mchango wa serikali Kuu bali pia wadau mbalimbali wa maendeleo na ambao wamekuwa wakisaidia katika eneo hilo.
Awali akifungua mkutano huo wa 49 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Idadi ya Watu na Maendeleo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema watu wasipohesabiwa wanatengwa na kwamba watu ni kiungo muhumu katika utekelezaji wa Agenda 2030.
Akaeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu yamejikita Zaidi katika usawa na kuwa takwimu za idadi ya watu, tathmini yake na uchambuzi wake ni muhimu sana katika kumaliza au kupunguza tofauti ya kati ya walionacho na wasionacho.Vilevile amesema takwimu sahihi zinasaidia katika kuwasaidia na kuwafikia watu walioko katika maeneo ambayo yahafikiki na hivyo kuwafikishia maendeleo na maisha yenye hadhi.

No comments:
Post a Comment