Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akifungua jengo la Maabara la Shule ya Sekondari ya
Mwakaluba katika jimbo la Kisesa akiwa aktika ziara ya mkoa wa Simiyu
Machi 5, 2016. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu , Dkt
Titus Kamani na Wazpili kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira, J. Mpina. (picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maabara ya Shule ya Sekondari ya
Mwakalubi katika jimbo la Kisesa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu
Machi 5, 2016 (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua shamba la pamba la mfano la mkulima
Gamuga Kimali kqtika kijiji cha Nandoya wilayani Meatu akiwa katika
ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipongeza Mama Anastazia Petro kwa kujifungua
salam motto wa kiume aliyepewa jina la Majaliwa wakati alipotembelea
Kituo cha Afya cha Mwandoya akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi
5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akiteta na Waganga na wauguzi wa Kituo cha Afya cha
Mwandoya wilayani Meatu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Kituo cha
Afya cha Nandoya wilayani Meatu baada ya kuzindua jengo la upasuaji na
kusalimia wagonjwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema atawatuma mawaziri watatu waje mkoa wa
Simiyu ili wakae na uongozi wa kila wilaya pamoja na wananchi ili
kubaini tatizo la mipaka baina ya wilaya hizo na Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza
na mamia ya wakazi wa vijiji vya Mwakaluba na Mwandoya akiwa kwenye siku
ya tano ya ziara yake mkoani Simiyu.
“Tangu
niingie hapa mkoani malalamiko ya mipaka nimeyapokea kila mahali
nilikopita. Nimeamua kuwatuma mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi; Waziri wa Maliasili
ua Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(TAMISEMI), Bw. George Simbachawene waje mkoa huu kutatua matatizo
yenu,” alisema.
“…Nitawatuma
waje na wapite kila wilaya, wakae na kuzungumza na wakulima na wafugaji
ili kubaini ni chanzo cha tatizo la migogoro hii kwenye mipaka ya
vijiji na hifadhi ya Serengeti. Pia Waziri wa TAMISEMI itabidi atoe
ufafanuzi kuhusu agizo lao la kutofanya shughuli yoyote mita 60 kutoka
kwenye mto Simiyu ili wananchi waelewe,” alisema.
Mapema,
Mbunge wa Kisesa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi (OMR – Mazingira)
alimweleza waziri Mkuu mbele ya wananchi hao kwamba limetolewa zuio
linalowakata wakazi wa mkoa huo wasifanye shughuli zozote umbali wa mita
60 kutoka kwenye kingo za mto huo.
“Limebandikwa
tangazo linalokataza wananchi waishio kando ya mto Simiyu wasifanye
chochote kuanzia Julai 30, 2016. Wananchi hawajashirikishwa wala
kuelezwa chochote zaidi ya kuona bango la matangazo tu. Watu
wananakatazwa wasichote maji wala kunywesha mifugo wakati hakuna
mabwawa, itawezekanaje? Tunaomba kauli yako kuhusu jambo hili,” alisema.
Ili
kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi hapa nchini, Waziri Mkuu alisema
Serikali ina mpango wa kuunda mabaraza ya ardhi 100 kwa nchi nzima
ambayo yatakuwa na jukumu la kutatua migogoro ya ardhi kwa wakati
Akitoa
taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Bw. Erasto Sima alisema
wilaya hiyo iliyoanzishwa Julai mosi, 1987 ina ukubwa wa kilometa za
mraba 8,835 ambapo asilimia 49 (sawa na kilometa za mraba 4,329) ya eneo
lote la wilaya hiyo ni hifadhi za wanyamapori.
Alilitaja
eneo hilo kuwa ni pori la akiba la Maswa, sehemu ya hifadhi ya
Serengeti, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na pori la hifadhi ya
usimamizi wa wanyama (WMA) la Makao na kwamba asilimia 51 iliyobakia
indiyo inayotumiwa kwa makazi ya watu, kilimo na malisho ya mifugo.
No comments:
Post a Comment