Wakiimba kupinga hatua hiyo. Msemaji wa jamii ya wafugaji Ismail Sevule (mweye kofia ya kijani) akiwa na wananchi.
Wananchi
jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba Mabango yenye ujumbe mbalimbali
wakipinga hatua ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala kurejesha
ardhi ya Shamba la Lokolova kwa chama cha Ushirika wa Wakulima ,wafugaji
na uzalishaji mali cha Lokolova.
Mifugo
ilikuwa sehemu ya mkusanyiko wa kuondi hilo la wananchi katika eneo hilo
ambalo mgogoro wake unatajwa kuwa ni wa zaidi ya miaka 30 sasa.
Wananchi
wakiongozana na mifugo wakiimba nyimbo mbalimbali kuonesha kupingana na
kauli ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ya kurejesha shamba hilo kwa
ushirika.
Wananchi wakipiga Push Up wakati wa mkusanyiko huo
.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MGOGORO
wa kugombea ardhi ya shamba la Lokolova lenye ukubwa wa ekari 2,470
lililopo kata ya Makuyuni wilaya ya Moshi vijijini umeibuka upya huku
wananchi jamii ya wafugaji wakimbebesha lawama mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Amosi hatua yake ya kutangaza kurejeshwa ardhi hiyo kwa
chama cha Ushirika wa Wakulima ,wafugaji na uzalishaji mali cha
Lokolova.
Mgogoro
huo wa zaidi ya miaka 30 sasa ,umeibuka baada ya kundi kubwa la wananchi
hao kukusanyika katika eneo hilo wakiwa na mifugo yao pamoja na mabango
yenye ujumbe mbalimbali huku wakiimba kuonesha kupinga hatua hiyo ya
serikali wakidai itachochea kuibuka kwa mgogoro uliokuwepo.
Februari
19 mwaka huu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Makala akiwa ameongozana na
viongozi wengine kutangaza maamuzi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya
mkoa kurejesha shamba hilo kwa Ushirika wa Lokolova hatua ambayo imefuta
mpango wa awali wa serikali ulioasisiwa na mtangulizi wake (Leonidas
Gama) wa kulifanya eneo hilo la ardhi litumike kujenga soko la kimataifa
na mji wa viwanda.
Katika
mkutano wake wa hadhara na wanachama wa chama cha ushirika cha Lokolova
pamoja na wananchi wa eneo hilo Makala aliweka bayana hatua zilizofikiwa
na kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichokutana Feb.12 Mwaka
huu Mjini Moshi kuwa Serikali imeridhia kurudisha shamba lenye ukubwa
wa ekari 2,470 kwa wanaushirika.
Kiongozi
wa wananchi Jamii ya wafugaji washio vijiji vya Lotima na Makuyuni
Ismail Sevule alisem katika tamko lao kuwa wanapinga hatua ya mkuu wa
mkoa (Makala) kurejesha ardhi hiyo ya Shamba la Lokolova kwa chama cha
Ushirika ,Ushirika ambao walida ulikwisha futwa tangu mwaka 2014.
“Tunatoa
tamko la kupinga hatua ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kurejesha ardhi ya
eneo la Lokolova kwa chama cha ushirika ,wanaushirika ambao si wa kata
ya Makuyuni ,watu hawa waliingia kwa mbinu katika ushirika uliokuwepo
,hata hivyo bado ushirika huu ulifutwa tarehe 1 4 ,mwezi wa tatu mwaka
2014 na kutangazwa katika gazeti la serikali la tarehe 23/5 mwaka 2014
“.alisema Sevule.
Alisema
wananchi jamii ya wafugaji wamepigwa butwaa kutokana na kauli ya mkuu
huyo wa mkoa huku wakieleza kutokubaliana na uamuzi huo wakitaka kujua
ushirika ulifutwa kwa vigezo gani na unarudishwa kwa vigezo na utaratibu
gani .
“Sisi
wananchi kata ya Makuyuni tunataka kujua ushirika ulifutwa kwa v igezo
gani na unarudishwa kwa vigezo gani ,mkuu wa wilaya ametangaza pia eneo
limesitishwa kilimo kwamba baada ya miezi mitatu wana ushirika watakuja
na Mastaer Plan yao ya kufanya kazi katika eneo hili,tunaiambia serikali
hatukubalina na utaratibu huo.”alisema Sevule katika tamko lao hilo.
“Hati
miliki ya eneo hili ilitolewa kinyemela mwaka ,1987,hati hiyo ilitolewa
wakati huo kukikiwa na mgogoro.watu wa ardhi walifanya makosa kutoa hati
wakati eneo likiwa na mgogoro ,tutaenda mahakamni kudai utolewaji wa
hati hiyo si halali”aliongeza Sevule.
Alisema
licha ya kuwepo kwa zuio la kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo
ikiwemo Kilimo ,wafugaji hao wameeleza kuendelea kulisha mifugo ya
katika eneo lilopewa jina la Phase 2 huku wakiongejea utaratibu wa
serikali juu ya matumizi katika eneo lililopewa jina la phace 1.
“Tunaomba
serikali ijue hivyo na kuanzia leo eneo hili tunaendelea kuchunga eneo
la phace 2 na phase 1 tunangojea utaratibu wa serikali….lakini
wakiingiza hawa wanaoleta Master plan tutapambana nao “alisema Sevula.
Akielezea
historia ya mgogoro huo mmoja wa wananchi hao, Hashim Mandale alisema
umeanza tangu mwaka 1983 hadi sasa huku akieleza kuwa wapo baadhi ya
wafanabiashara na viongozi ndio wanaasisi mgogoro huo.
“Eneo
hili liko ndani ya vijiji viwili vya Lotima na Makuyuni ,tulipo zaliwa
sisi,kulianzishwa Ushirika wa wafugaji ambapo walitoa ng’ombe, eneo hili
likagawanywa Phace 1 na Phase na eneo la phase 1 watu wote wa Tambarare
tuliridhia kulitoa kwa serikali kwa ajili ya kujenga soko la
kimataifa.”alisema Mandali.
“Tunashangazwa
leo hii tumekuja kuona maeneo yote mawili yanachanganywa na kuwa kitu
kimoja na hawa watu wana sema ni eneo la ushirika na warudishiwe wana
ushirika maana yake mkuu wa mkoa ndiye atakua ameanzisha upya mgogoro
huu.”aliongeza Mandali.
Mwenyekiti
wa chama cha Ushirika huo ,Samwel Lyimo alisema anavyotambua yeye
hakuna mgogoro kati ya Wakulima na Wafugaji katika eneo hilo isipokuwa
kuna watu ambao wamevamia eneo na kufanya shughuli za kulisha mifugo
yao.
Tangu
mwaka 2011 serikali mkoani Kilimanjaro ilikusudia kulitaifisha shamba
hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari elfu 2,470 ili kuepusha mgogoro wa
ardhi baina ya wakulima na wafugaji wa maeneo ya Lotima na Makuyuni
waliokuwa wakigombania shamba hilo la Lokolova kwa ajili ya Kilimo na
Malisho.
No comments:
Post a Comment