Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akizungumza na menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kuzitambua taasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akiongea wakati wa kikao na wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TBA Arch.Elius Mwakalinga.
Wafanyakazi wa Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (hayupo katika picha) leo
jijini Dar es Salaam, katika ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
Mhandisi. Manase Ole Kujan katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo
chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi
hizo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (Kushoto)
akifafanua jambo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi
(NCC) Mhandisi.Julius Mamilo(kulia) wakati ziara yake ya kuzitambua
tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu
yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam.
Wafanyakazi
wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani(Hayupo katika picha)
Mamilo katika
ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa
kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es
Salaam.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (UJENZI).
NAIBU
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani,
amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uadilifu,
bidii na kwa uharaka ili kuendana na kasi ya madiliko ya Serikali ya
awamu ya Tano.
Ameyasema
hayo wakati alipofanya ziara katika taasisi zilizo chini ya Wizara yake
ikiwemo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa lengo la kupata mafunzo
ya kiutendaji katika taasisi hizo.
Aidha
amezitaka taasisi hizo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vya
mapato walivyonavyo na kamwe kutotegemea ruzuku kutoka Serikalini.
“Nataka
ifikapo mwaka wa fedha ujao makusanyo ya mapato yawe yameongezeka zaidi
kuliko matumizi na kamwe msikae kusubiri ruzuku kutoka Serikalini,
kikubwa ni kubuni vyanzo vyengine vya mapato ili kuweza kujiendesha”,
alisema Naibu Waziri.
Hata hivyo
Naibu Waziri huyo amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa weledi na
bila woga kwani Serikali haitamuonea huruma yeyote anayekiuka kutekeleza
wajibu wake.
“Nawaomba
mfanye kazi kwa morali kubwa ili kuweza kuisaidia jamii ambayo
inahitaji huduma muhimu kutoka Serikalini”, alifafanua Eng. Ngonyani.
Katika
hatua nyingine Eng. Ngonyani amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA
Eng. Manase Ole kujan kutatua changamoto walizonazo ili kuleta
mabadiliko chanya katika taasisi hiyo.
“Una
nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko hasa katika mfumo mzima wa
ukatikatishaji tiketi eneo la Magogoni ambalo limekuwa kero katika mfumo
mzima wa ukusanyaji wa mapato”, alisisitiza Naibu Waziri Ngonyani.
Sambamba
na hilo Naibu Waziri amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo
Tanzania Arch. Elius Mwakalinga, kuandaa taarifa ambayo itaonyesha
idadi ya nyumba za Serikali wanazomiliki na ibainishe taarifa ya
watumishi wenye stahili ya kupangishwa kwenye nyumba hizo.
Kwa
upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole Kujan amesema
wakala huo umepanga kuboresha miundombinu hasa katika usafiri wa majini
na kuhakikisha inapunguza changamoto ya usafiri katika vivuko.
Naye
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Eng. Julius
Mamilo amebainisha changamoto walizonazo ikiwemo uhaba wa fedha hali
inayosababisha Baraza hilo kukwama katika kufanya kazi katika miradi
yake ya maendeleo hususan katika kufanya kazi za utafiti.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (SEKTA YA UJENZI)
No comments:
Post a Comment