Mbowe Amtosa Zitto Kabwe Baraza La Mawaziri - LEKULE

Breaking

6 Feb 2016

Mbowe Amtosa Zitto Kabwe Baraza La Mawaziri



Kambi rasmi ya upinzani bungeni, imetangaza baraza lake la mawaziri kivuli ambalo Chama cha ACT Wazalendo, chenye mbunge mmoja, Kabwe Zitto, ndicho hakikuingizwa kwenye baraza hilo. Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe alitangaza jana bungeni baraza hilo.

Chadema chenye wabunge wengi katika kambi hiyo, kina mawaziri vivuli wengi ikilinganishwa na vyama vingine na wakati huo huo, kina wizara nyingi ambazo kinaongoza peke yake kwa maana ya kuwa na mawaziri na naibu mawaziri vivuli.

Mbowe alisema idadi ya wizara alizotangaza inafanana na ya wizara za Serikali ya Awamu ya Tano ambazo zipo 19.


Mbali na kutangazwa kwa majina hayo ,Bunge lilifanya uchaguzi wa wajumbe wa kuliwakilisha kwenye taasisi mbalimbali za kibunge.

Wajumbe hao ni wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Bunge la Afrika (PAP), Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF), Kamati ya Utendaji wa Bunge la Jumuiya ya Madola (CPA) na Umoja wa Wabunge Duniani (IPU).

 Akitangaza wabunge walioshinda katika uchaguzi huo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema idadi ya wajumbe waliorudisha fomu za kuwania nafasi hizo ilikuwa inalingana na idadi ya nafasi zilizokuwa zikiwaniwa, hivyo kuwafanya wote kupita bila kupigiwa kura.

1.Tume ya Utumishi wa Bunge Kangi Lugola, Fakharia Shomar Khamis, Mary Chatanda, Mussa Azzan Zungu, Salim Hassan Turky, Magdalena Sakaya na Peter Msigwa.

2.Bunge la Afrika Mboni Mhita, Asha Abdullah Juma, Dk Faustine Ndugulile, Stephen Masele na David Silinde.

3.Jukwaa la Wabunge wa SADC Jamal Kassim Ali, Esther Mmasi, Selemani Zedi na Ally Abdallah Saleh.

4.Kamati ya Utendaji ya Bunge la Jumuiya ya Madola Amina Mollel, Maria Kangoye, Zainab Vullu, Khamis Mtumwa Ali, Salum Rehani, Japhet Hasunga, Josephat Kandege, Dk Raphael Chegeni, Jitu Soni, Immaculate Semesi, Juma Hamad Omar na Tundu Lissu.

5.Umoja wa Mabunge Duniani Dk Pudenciana Kikwembe, Juma Othman Hija, Mohamed Mchengwerwa, Peter Serukamba na Susan Lyimo. 

No comments: