CUF: Maalim Seif Sharif Hamad Akishinda Uchaguzi wa Marudio Zanzibar Hatakubaliana Na MatokeoChama cha Wananchi (CUF) kimesema ikitokea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad ameshinda kwa kupigiwa kura na akaibuka mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, hatakwenda kuapishwa. 
 
Kimesema kuna uwezekano mkubwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ikaweka jina la Maalim, wawakilishi na madiwani katika karatasi za kupigia kura na kusisitiza, ikitokea hivyo na wagombea hao wakapigiwa kura, wote hawataenda kuapa.

“Kama wagombea wetu wakichaguliwa na ZEC ikawatangaza washindi itakuwa ni kazi bure. Pia, CUF hatutakwenda mahakamani kufungua kesi ya kikatiba kupinga hatua ya mwenyekiti wa ZEC kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,” Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui aliwaambia waandishi wa habari jana.

Oktoba 28, mwaka jana mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi wa rais, wawakili shi na madiwani kwa maelezo kuwa sheria na kanuni zilikiukwa na baadaye kutangaza Machi 20 kuwa siku ya kupiga kura upya.

Mazrui alisema licha ya CUF kuiandikia barua ZEC, ikitaka wagombea wake wote kuondolewa katika orodha ya karatasi ya kupigia kura, kuna uwezekano mkubwa wa majina hayo kutoondolewa.

“... Sisi tumeshaipelekea ZEC barua 54 za wawakilishi na madiwani walioshindwa au kushinda katika uchaguzi wa Oktoba 25 na kuwaeleza kuwa wawaondoe katika karatasi za uchaguzi wa marudio. 

"Hata kama wananchi watamchagua Maalim Seif kwa asilimia 90 hawezi kwenda kuapishwa. Kufanya hivyo ni sawa na kukataa kula nyama ya nguruwe lakini mchuzi wa nyama hiyo unaunywa.” 

Mazrui ambaye alitangazwa mshindi wa uwakilishi wa jimbo la Mtopepo, kabla ya kufutwa kwa matokeo hayo alisema, “Hatuna shida na uchaguzi wao, tumekosa nini mpaka tuwe na shida nao?” 

Alisema CCM inadhani kwamba CUF itajitosa kushiriki uchaguzi huo wa marudio katika dakika za mwisho; “wanachotakiwa kujua ni kwamba hatuingii katika uchaguzi wao wawe na amani yote.” 

Akizungumzia kauli ya Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu kwamba CUF walipaswa kupinga kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi, siku 14 baada ya kutangazwa, Mazrui alisema kauli hiyo imedhihirisha kuwa hata wakienda mahakamani hakuna haki itakayotendeka.

“Ameshatoa hukumu kabla hata kesi haijafunguliwa. Muda wa siku 14 aliousema unahusu ukomo wa kupeleka kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu. Kesi ya uchaguzi msingi wake mkubwa ni uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi ambao CUF na wajumbe wateule hatuna tatizo nao,”
alisema.

“Hakuna anayetaka atangazwe mshindi kati ya wagombea wote wa CUF kwa kuwa walitangazwa kihalali na wasimamizi wa uchaguzi na kupewa vyeti. 

"Aliyehujumu uchaguzi si ZEC ni Jecha. Sisi kesi tunayoweza kufungua ni ya kikatiba si kupinga matokeo na kesi ya kikatiba haina muda wa kufungua kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.” 

Alisema kutokana na kauli ya Makungu, CUF imewashauri wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliokuwa na nia ya kupeleka shauri mahakamani kuachana na wazo hilo kwa maelezo kuwa Jaji Makungu ameshaandaa hukumu na kuisoma hadharani.
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF