Boko Haram ni wanafunzi wa Al shabab - LEKULE BLOG

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 15 February 2016

Boko Haram ni wanafunzi wa Al shabab

Image copyrightBoko Haram video
Image captionRais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema kuwa anaushahidi wa kutosha kuwa wapiganaji hao wa Boko Haram walijifunzia ugaidi nchini humo.
Wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram wanaosababisha maafa mengi nchini Nigeria walijifunza ukatili wao kutoka kwa al Shabab nchini Somalia.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema kuwa anaushahidi wa kutosha kuwa wapiganaji hao wa Boko Haram walijifunzia ugaidi nchini humo.
''Magaidi wanauhusiano na kila mara wanasaidiana kubadilishana mbinu na mawazo ya kuetekeleza maafa zaidi'' alisema rais Mohamud.
''Jamii ya kimataifa haina budi ila kuisaidia Somalia kupamabana dhidi ya Al Shabaab'' aliongezea rais huyo.
''Bila shaka tunaushahidi mkubwa kuwa Boko Haram ni wanafunzi wa Al Shabab''
Image copyrightAP
Image caption''tunaushahidi mkubwa kuwa Boko Haram ni wanafunzi wa Al Shabab'' rais Mohamud
''Iwapo Somalia itapata amani Afrika bila shaka itakuwa na amani'' aliongezea rais huyo.
Rais Hassan Sheikh Mohamud aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa usalama wa kimataifa uliokamilika mjini Munich Ujerumani siku ya Jumapili.
Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages