Uongozi wa klabu ya Simba usiku wa January 11 kuingia 12 unatajwa kufanya maamuzi magumu, kutokana na mwendo wa timu yao kwa sasa, stori kutoka mtandao wa mwandishi na mchambuzi wa soka Tanzania Salehjembe.blogspot.com, umeripoti uongozi wa klabu ya Simba kuamua kumfuta kazi kocha wake wa kiingereza Dylan Kerr.
Simba ambayo ilitolewa na Mtibwa Sugar katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2016 kwa goli 1-0, dalili za kuwa kocha Kerr yupo katika wakati mgumu, zilianza kuonekana baada ya afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara kufunguka kwa jazba kuwa yeye kama shabiki ameshangazwa na maamuzi ya mwalimu ya kutopanga mapema kikosi cha kwanza. Kerr anatajwa kuitwa kwenye kikao cha dharura lakini kikao ambacho kinatajwa kuwa tayari kina maamuzi.
Haji alikuwa akiongea baada ya mchezo akijitaja kwa kiasi kikubwa kama shabiki na sio kiongozi wa Simba, ili apate nafasi ya kutoa ya moyoni, hiyo ni moja kati ya dalili za Kerrkuwa alikuwa anawashiwa taa nyekundu. salehjembe.blogspot.com umeripoti nukuu chache za chanzo cha siri kuwa Kerr amefutwa kazi, nafasi yake itachukuliwa naJackson Mayanja ambaye hivi karibuni alisaini mkataba wa kuwa kocha msaidizi, lakini sasa ataava viatu vya Kerr.
No comments:
Post a Comment