Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa
akizungumza jambo wakati wa kikao cha utambulisho wa viongozi wapya wa
Wizara. Kikao hicho kimeshirikisha Menejimenti ya Wizara, Taasisi zilizo
chini ya Wizara zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la
Maendeleo ya Petroli la Tanzania (TPDC), Wakala wa Ukaguzi wa Madini
(TMAA), Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma
(MRI) na Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Katikati
ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akimsikiliza
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala
ya Madini, Profesa James Msofe wakati wa kikao cha utambulisho wa
viongozi wapya Wizarani. Wengine kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara
Profesa Justin Ntalikwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara anayeshughulikia
masuala ya Nishati, Dkt. Eng. Juliana Pallangyo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
(katikati), akizungumza jambo wakati wa kikao cha utambulisho wa
viongozi wapya wa wizara ambacho kiliongozwa na Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Kikao hicho kimeshirikisha Menejimenti
ya Wizara, Taasisi zilizo chini ya Wizara zikiwemo Wakala wa Nishati
Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli la Taifa (TPDC), Wakala
wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Wakala
wa Jiolojia Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Chuo
cha Madini Dodoma (MRI) na Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa
(NDC).
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati)akimweleza
jambo Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Oforo Ngowi wakati wa kikao
cha utambulisho wa viongozi wapya wa wizara. Kikao hicho kimeshirikisha
Menejimenti ya Wizara, Taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwemo Wakala wa
Nishati Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli la Taifa
(TPDC), Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Shirika la Umeme Nchini
(TANESCO), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI) na Mtendaji kutoka Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC).
Mkurugenzi
Msaidizi wa RasilimaliWatu, Caroline Musika akiongea jambo wakati wa
kikao cha utambulisho wa viongozi wapya wa Wizara. Katikati ni Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Kikao hicho kimeshirikisha
Menejimenti ya Wizara, Taasisi zilizo chini ya Wizara zikiwemo Wakala
wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli la Tanzania
(TPDC), Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Shirika la Umeme Nchini
(TANESCO), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI) na Mtendaji kutoka Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC).
Baadhi
ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakifuatilia kikao baina
ya Menejimenti ya Wizara, Taasisi zilizo chini ya Wizara zikiwemo
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli la
Tanzania (TPDC), Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Shirika la Madini
la Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI) na Mtendaji kutoka
Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
Picha Chuo cha Madini Dodoma
Na Asteria Muhozya.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo amewataka Watendaji wa Wizara,
Wakuu wa Taasisi zilizochini yake na watumishi wote kufanya kazi kwa
bidii kuhakikisha kwamba sekta za Nishati na Madini zinakuwa na manufaa
makubwa kwa Taifa ikiwemo mabadiliko kiuchumi kupitia sekta hizo.
Profesa
Muhongo ameyasema hayo wakati wa kikao cha utambulisho wa viongozi
wapya wa Wizara kilichoshirikisha Menejimenti ya Wizara, Taasisi zilizo
chini yake zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la
Maendeleo ya Petroli la Tanzania (TPDC), Wakala wa Ukaguzi wa Madini
(TMAA), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI) na Watendaji kutoka Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC).
“Ni lazima tujitume, hili ndio jukumu letu la kwanza. Wananchi
wanataka umeme na wanataka mabadiliko kupitia sekta za nishati na
madini. Tufanye kazi kwa umoja na uwazi kwasababu tumepewa fursa ya
kuwatumikia wananchi hivyo ni lazima tubadilike na mabadiliko ni lazima.
Asiyeweza kuendana na kasi ya awamu hii aondoke, hakuna atakayeonewa,”
ameongeza Prof. Muhongo.
Prof Muhongo aliongeza kuwa, kutokana na uzoefu wa viongozi hao na
watendaji wa Wizara na Taasisi anaamini kuwa yatakuwepo mabadiliko
katika sekta hizo kutokana na sifa zao kitaaluma na kiutendaji.
“Wananchi wana imani kubwa na uteuzi wetu na uwepo wetu katika wizara.
Tufanye kazi kwa manufaa ya Taifa”, amesema prof. Muhongo
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Justin Ntalikwa
alieleza kuwa, uongozi huo unatarajia kufanya kazi kwa uadilifu na
umakini na kuongeza kuwa, “ jukumu lililo mbele yetu ni kubwa tunahitaji
kufanya kazi kwa bidii tukitumia uzoefu, wote kutekeleza majukumu
yaliyo mbele yetu”,amesema Profesa Ntalikwa.
Naye, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Madini,
Profesa James Msofe, amesema kuwa, aanatarajia kujifunza kwa kasi kubwa
majukumu yake ili kuweza kufikia matarajio ya wananchi na taifa.
No comments:
Post a Comment