Kocha
wa Bayern Munich, Pep Guardiola (pichani) amesema anataka kupata
changamoto mpya katika maisha yake ya soka na anataka kwenda kufundisha
Uingereza baada ya kugoma kuongeza mkataba Bayern Munich na nafasi yake
kuchukuliwa na Carlo Ancelotti.
Vilabu
vya Manchester United, Mancheter City na Chelsea vyote vya Uingereza
tayari vinaonekana kumuhitaji kocha huyo wa zamani wa Barcelona ambaye
anaonekana kupata mafanikio kwa klabu zote ambazo amekuwa akizifundisha
hali inayovifanya vilabu vingi kuhitaji kumpata kocha huyo raia wa
Hispania.
Guardiola
ameweka wazi mipango yake ya kufundisha klabu za Uingereza katika
mkutano wake na waandishi wa habari na kusema kuwa anataka kupata
changamoto mpya ya soka na anapendelea kwa sasa kufundisha klabu za
Uingereza.
“Nahitaji
changamoto mpya na ninataka kutumia nafasi hiyo kuwa meneja wa klabu za
Uingereza, nataka kuzoea hali ya Uingereza na kuangalia mbele zaidi
katika viwanja, nina miaka 44 kwa sasa nadhani ni muda sahihi lakini
bado sijasaini kwa klabu yoyote, nitakapopata klabu mpya nitaweka wazi
ili kila mtu aijue,” alisema Guardiola.
Aidha
baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikimuhusisha kocha hiyo na klabu
ya Manchester City ambayo nayo inatajwa kumuhitaji kocha huyo pamoja na
wapinzani wao Manchester United na Chelsea ambayo wiki kadhaa zilizopita
walimtimua aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho na kumchukua
Guus Hiddink kwa mkataba wa muda mfupi hadi utakapomalizika msimu wa
2015/2016.
Baada
ya Manchester City kuhusishwa zaidi na Guardiola, Kocha wa Man City,
Manuel Pellegrini ameulizwa na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa
Guardiola kutaka kufanya kazi Uingereza na kujibu “Sina uamuzi wowote
kuhusu hilo au hata kuhusu mameneja wengine,” alisema na kuongeza “Ni
swali ambalo nililijibu wiki mbili zilizopita wakati niliposema siyo
sahihi kuhusu hilo [Guardiola kuchukua nafasi yake]”
No comments:
Post a Comment