Mshitakiwa
wa kwanza katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi ameripotiwa kufariki akiwa
gerezani, siku chache kabla ya kesi kusikilizwa.
Taarifa
ya kifo cha mshtakiwa huyo aliyetajwa kwa jina la Chibago Chiuguta
mwenye umri wa miaka 33, zilitolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu na kueleza kuwa mshitakiwa huyo alikutwa akiwa amekutwa na
umauti.
Kufuatia
taarifa hizo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Thomas Simba
aliagiza upande wa Magereza kuhakikisha wanafuatilia cheti cha kifo cha
mshitakiwa huyo.
Marehemu
alikuwa kati ya washtakiwa 11 waliodaiwa kumuua Dk. Mvungi katika eneo
la Msakuzi, Kiswegere katika wilaya ya Kinondoni. Washtakiwa hao
wanadaiwa kufanya kosa hilo Novemba 3 mwaka 2013.
Upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment