Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwasili mkoani Geita na akakutana na uongozi wa mkoa huo ambapo alisisitiza suala la wananchi kunufaika na mgodi wao wa dhahabu wa Geita Gold Mine.…
"Wakati
nilipopita kwenye kampeni nilipita kwenye mgodi wa Geita Gold Mine
nikaangalia hali ya watu wa Geita nikawa na majonzi makubwa…sikuridhika
kuwa na mgodi mkubwa kama ule na hali ya watu wa Geita iko ilivyo hivi
nikawa sikuridhika nilikuwa mkali kidogo." Alisema Mama Samia na kuongeza;
"Wakati
naangalia presentation nimeona amount nzuri kidogo inatolewa kwenda kwa
watu ingawa bado ninamaswali yangu ambayo nitayafanyia kazi ili tuone
ni kiasi gani sahihi kinatakiwa kutolewa na mgodi kwenda kwa wananchi,
dhahabu iliyopo niyawana Geita Mungu amewaumbia katika ardhi yao
"Hatukatai
kuwa na wawekezaji wachimbe lakini uchimbaji uwe na faida kote wao
wapate na wananchi wapate kwa hiyo hatunabudi kusimamia vizuri na
kuhakika kwamba wananchi wa Geita wanafaidika na rasilamali ambayo
Mwenyezi Mungu amewapangia."
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa wakati alipowasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa GGM Mkoani Geita jana Januari 04,2016 kwa
ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya
maendeleo Mkoani humo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na baadhi ya wawekezaji wa Mgodi wa GGM Mkoani Geita
alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita jana Januari 04, 2016 kwa ajili
ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya
maendeleo Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa akizungumza wakati akitoa Taarifa ya
Maendeleo ya Mkoa wa Geita, kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia), katika kikao kilichofanyika
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, jana Januari 4,
2016. Katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Injiani Gerson Lwenge.
No comments:
Post a Comment