Lowassa na Maalim Seif Wajifungia Dodoma Kujadili Hatma Ya Zanzibar la Sakata la Wabunge wa UKAWA Kugomea Kamati za Bunge - LEKULE

Breaking

25 Jan 2016

Lowassa na Maalim Seif Wajifungia Dodoma Kujadili Hatma Ya Zanzibar la Sakata la Wabunge wa UKAWA Kugomea Kamati za Bunge



Viongozi wa juu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Edward Lowassa na wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, walijifungia mjini hapa Dodoma kujadili mambo mawili mazito.

Kwa mujibu wa taarifa toka ndani ya kikao hicho, viongozi hao walijadili mustakabali mzima kuhusu kutangazwa kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Machi 20, mwaka huu pamoja na uamuzi wa wabunge wao kugomea Kamati za Bunge.

Aidha, viongozi hao baada ya kufikia uamuzi, jana usiku walikuwa na mkutano na wabunge wa Ukawa kuwaeleza uamuzi waliofikia na nini wanachotakiwa kukifanya wakiwa bungeni.

"Ni kweli viongozi wa juu wamejadili mambo makubwa mawili, hatma ya uchaguzi wa Zanzibar na kuhusu Kamati za Bunge zilivyoundwa, taarifa kamili mtaipata baadae" kilieleza chanzo

No comments: