Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema misaada inayotolewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jamii ni lazima iwe imekidhi viwango vya ubora, hivyo haitakiwi kuangaliwa kwa vigezo vya dini, itikadi wala siasa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu huyo wakati akizungumza na waandishi
wa habari ofisi kwake baada kituo kimojwapo nchini kukataa misaada
iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA), Wilfred Lwakatare hivi
karibuni.
Dkt. Ulisubisya alisema hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari hapa
nchini viliripoti kwamba misaada iliyotolewa na Mbunge huyo, katika
baadhi vituo afya Zahanati kwa ajili ya wajawazito ilikataliwa.
“Serikali
ina sera ya kusaidia jamii hususan misaada inayotolewa kwenye huduma za
afya, ambayo inakidhi viwango vya ubora kulingana Sheria , kanuni na
taratibu za Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),” alisema Katibu Mkuu huyo.
Hivi karibuni iliripotiwa kwamba baadhi ya wakuu
wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma
kupokea msaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na mbunge wa Chadema kwa madai ya
kupewa maelekezo na Serikali.
Dkt. Ulisubisya amewataka watendaji wa afya
wa vituo hivyo wasiangalie misaada hiyo kwa misingi ya dini,
itikadi na kisiasa.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo amewataka watu mbalimbali wenye lengo la
kutoa misaada katika vituo vya afya kuhakikisha kwamba imekidhi viwango
viliyowekwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Katika hatua nyingine
aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando amekabidhi
ofisi hiyo kwa Katibu Mkuu huyo mpya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (kulia) akikabidhiwa nyaraka muhimu na aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Donan Mmbando.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (kulia) akikabidhiwa nyaraka muhimu na aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Donan Mmbando.
No comments:
Post a Comment