Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifunua pazia
kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Tiba na
marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za kulevya hapo Kidimni,
Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unaguja.
Balozi
Seif pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Dr. Omar Dadi Shajak wa kwanza kutoka kulia na Mkuu wa Mkoa wa
Kusini Unguja Dr. Idriss Muslim Hijja nyuma yake wakifurahia na kupiga
kofi mara tu baada ya Balozi Seif kuweka jiwe la msingi la Kituo cha
Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana hapo Kidimni.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Shajak wa pili
kutoka kushoto akimpatia maelezo Balozi Seif wa kwanza kutoka kushoto
jinsi ya ujenzi wa kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana
utakavyoendelea hapo Kidimni.Wa Pili kutoka kulia ni Mkandarasi wa
ujenzi huo kutoka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar Nd.
Mbwana Bakari juma.
Baadhi
ya wananchi walioshiriki hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la Kituo
cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za kulevya
hapo Kidimni Wilaya ya Kati.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Omar Dadi Shajak
akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia
kwa Vijana hapo Kidimni Wilaya ya Kati.
Balozi
Seif akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Kituo
cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana ikiwa ni shamra shamra za
kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika
sasa katika kuona Wananchi wanalazimika ipasavyo kutoa mashirikiano ili
kusaidia kufanikisha ile azma ya Serikali Kuu ya kupambana na biashara
na matumizi ya dawa za kulevya Nchini.
Amesema
kuwa kukosekana ushirikiano katika kutoa ushahidi Mahakamani dhidi ya
watu wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya ambako kunawahusu zaidi
Wananchi walio karibu na wahusika hao inapelekea kufutwa kwa kesi na
hivyo kudumaza juhudi za Serikali katika vita dhidi ya matumizi ya dawa
hizo.
Balozi
Seif Ali Iddi amesema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa
Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za
kulevya hapo Kidimni, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unaguja ikiwa ni
shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi
ya Zanzibar ya Januari 1964.
Amesema
suala la Dawa za kulevya hivi sasa limekuwa janga la Dunia kwa vile ni
la muda mrefu na kuathiri watu wengi hasa Vijana. Hivyo udhibiti wa
matumizi yake unahitaji maamuzi magumu ya Serikali pamoja na ushirikiano
wa Kitaifa, Kikanda na Dunia kwa ujumla.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwanasihi walioanzisha nyumba hizo pamoja
na Vijana wanaoishi kwenye nyumba hizo kujitahidi kutoshawishika kurudi
nyuma kwa kujiingiza tena katika janga la matumizi ya dawa za kulevya.
Mapema
akitoa Taarifa ya ujenzi wa Kituo hicho Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr.Omar Dadi Shajak alisema ujenzi wa kituo
hicho unagharimiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa zaidi ya
Shilingi Bilioni Nne na Milioni Mia Mbili { 4,200,000,000/- } hadi
kukamilika kwake.
Dr.
Shajak alisema Kituo hicho cha aina yake ndani ya ukanda wa Mwambao wa
Afrika Mashariki kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Vijana wapato 200 wake
kwa waume kwa wakati mmoja ambapo pamoja na mambo mengine kutakuwa na
mafunzo ya kazi za amali, michezo na huduma nyengine za kurekebisha
tabia.
Dr.
Omar Dadi Shajak amewafahamisha kwamba Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar katika kukabiliana na wimbi la uingizaji, uuzaji na
matumizi ya dawa za kulevya tayari imeshaandaa zawadi kwa Mtu au Kikundi
kitakachojitolea kutoa Taarifa ya kukamatwa kwa wahusika wa dawa za
kulevya.
Ujenzi
wa Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za
kulevya hapo Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja chenye eneo la
ukubwa wa Eka Tatu kinajengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Al – Hilal
General Trading Cooperation Limited chini ya Mkandarasi Mbwana Bakari
Juma kutoka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar.
No comments:
Post a Comment