WAZIRI DKT. MAHIGA ATEMBELEA KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA CHA AICC JIJINI ARUSHA - LEKULE

Breaking

21 Dec 2015

WAZIRI DKT. MAHIGA ATEMBELEA KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA CHA AICC JIJINI ARUSHA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa ,Balozi Augstine Mahiga amesema eneo la Laki Laki lililopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha lililotengwa kwaajili ya ujenzi wa taasisi za kimataifa utaifanya Tanzania kung'ara duniani.

Balozi Mahiga alisema hayo Desemba 19 baada ya kufanya ziara kwenye eneo hilo na Kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC .

Eneo hilo litajengwa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari(MICT)Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR) na taasisi zingine na kusema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.

Akiwa kwenye kituo cha AICC alipokea taarifa za mradi wa ujenzi wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Kilimanjaro International Convention Center kitachovuta dunia Tanzania.

Pia Waziri alizungumzia hali ya kisiasa nchini Burundi kuwa inaigusa Tanzania na kuwa atawasiliana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera kuandaa kuandaa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje.

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga(kulia)akiwasili kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha International Conference Center(AICC) ambacho ni sehemu ya Wizara hiyo,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AICC,Elishilia Kaaya. 
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga akisaini kitabu cha wageni. 
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha International Conference Center(AICC)Elishilia Kaaya(kulia) akifafanua jambo mbele Waziri Mahiga(kushoto)katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha International Conference Center(AICC)Elishilia Kaaya akifafanua jambo mbele Waziri Mahiga(wa pili kulia)wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku(kulia)Mwenyekiti wa Bodi ya AICC,Balozi Christopher Lihundi(aliyevaa tai) na Mkuu wa mawasiliano serikalini,Mindi Kasiga. 
 
Mwenyekiti wa Bodi ya AICC,Balozi Christopher Lihundi akizungumza jambo mbele Waziri Augustine Mahiga aliyefika katika kituo hicho tangu ateuliwe kushika wadhifa huo. 
 
Baadhi ya watumishi wa AICC.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga akizungumza na wajumbe wa Bodi ya AICC na watumishi wa kituo hicho ,kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya AICC,Balozi Christopher Lihundi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku.
 
Mkuu wa mawasiliano serikalini, Mindi Kasiga akiongoza kipindi cha maswali kwa waandishi wa habari.

No comments: