Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amekutana naMakamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad,
leo tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam kufuatia maombi
yake ya siku nyingi.
Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi hawa kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed
Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya
uelewano Zanzibar.
Rais
Magufuli pia amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa
kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF
na CCM yakiendelea huko Zanzibar.
Katika
Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif
Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya
siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku
akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane.
Majadiliano
yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya
nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu
ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema.
Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea
kudumishwa Zanzibar.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
21Desemba, 2015
No comments:
Post a Comment