Madiwani wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wamemtetea Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty 7aliyesimamishwa kazi.
Mhandisi
Natty alisimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kusiamia vyema mkataba
wa ubinafsishaji wa ufukwe wa Coco Beach kwa diwani wa Mbagala Yusuf
Manj pamoja na kutowasimamia ipasavyo watumishi wake na kupelekea ujenzi
wa baadhi ya barabara za manispaa hiyo chini ya kiwango.
Katika
utetezi wao, madiwani hao wameeleza kuwa Mhandisi Natty amewajibishwa
kisiasa zaidi kwa kuwa wakati wa uingiaji wa mkataba wa Coco Beach yeye
alikuwa bado hajawa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.
Katika
tamko lao, madiwani hao wameitaka serikali ya awamu ya tano
kushughulikia mgogoro huo na kuangalia hatua za kisiasa zilizochukuliwa.
Pia, waliahidi kuwa endapo watafanikiwa kushika manispaa hiyo
watahakikisha maeneo yote ya umma yanakuwa katika hali salama na
yanaufaidisha umma.
Mbali
na tamko la madiwani hao, Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akiwa
na diwani wa kata ya Ubungo, Boniphace Jacob (Chadema), walionesha
mikataba iliyoingiwa kati ya Manispaa ya Kinondoni na Yusuf Manji ambayo
inaonesha kuwa wakati huo Natty hakuw Mkurugenzi wa manispaa hiyo.
Walidai kuwa sababu zilizotumika ni za kisiasa kwakuwa mkugenzi huyo
alitenda haki na kupelekea majimbo ya uchaguzi kuchukuliwa na Chadema.
“Kama
kuna ufisadi umetokea hatutamtetea mtu na kama kuna mtu tunaona
anaonewa hatutakaa kimya na hili la Natty tunamwomba Rais John Magufuli
aunde tume ambayo haitawahusisha Tamisemi na wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
No comments:
Post a Comment