Aliyekuwa
mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na Ukawa, Edward
Lowassa amesema anashangaa kuona anaambiwa mleta vurugu wakati dunia
inamkubali kuwa ni mlinzi wa amani.
Kauli
ya Lowassa imekuja ikiwa ni siku moja baada ya taasisi za kidini 1,200
duniani kupitisha jina lake kwa ajili ya kumpatia Tuzo ya Amani.
“Nimepokea
kwa unyenyekevu na furaha tuzo ya amani duniani ninayotarajiwa kupewa
na taasisi za kidini 1200 duniani,” alisema Lowassa akinukuliwa na
msemaji wake, Aboubakar Liongo.
Lowassa alisema tuzo hiyo ni kithibitisho cha uongo wa CCM na Serikali yake kuwa wapinzani ni watu wa vurugu.
Taasisi
hizo katika kikao chake huko Bukavu DR Congo, zilitangaza kumpa tuzo
hiyo Edward Lowassa kutokana na utulivu aliyouonyesha kabla na baada ya
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Taarifa
ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu Kwa
jamii, Mchungaji William Mwamalanga ilisema kiasi wajumbe 1,400 wa
mkutano huo kutoka kote duniani walikubaliana kumpa tuzo hiyo Lowassa
kati ya wanasiasa 1,000 waliyoshindanishwa ili kumpata kiongozi bora wa
Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya
madaraka.
Alisema
yeye ni muungwana na ana hofu ya Mungu na hata siku moja hatoweka mbele
maslahi binafsi, na ndiyo maana aliwatuliza wananchi waliyokuwa
wakimtaka kutoa tamko baada ya matokeo kutangazwa.
“Siko
tayari kuingia Ikulu huku mikono yangu ikibubujika damu. Nashukuru
taasisi hizo za kidini duniani, zimeliona hilo,” alisisitiza Lowassa.
No comments:
Post a Comment