Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akihutubia kwenye mahafali ya kwanza
ya Shahada ya Takwimu Rasmi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika
kilichopo maeneo ya Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akiwa kwenye maandamano na wahitimu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo maeneo ya
Changanyikeni jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho,
Professa Innocent Ngalinda.
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akiwa kwenye picha ya pamoja na
viongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika pamoja na wahitimu wa
Shahada ya kwanza ya Takwimu Rasmi katika chuo hicho kilichopo maeneo ya
Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
KATIBU
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amevitaka vyuo na taasisi za elimu
nchini kuhakikisha vinatoa mafunzo bora yanayoendana na mahitaji ya soko
la ajira.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika mahafali ya kwanza ya Shahada ya Takwimu
Rasmi katika Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Sefue
amesema ni vyema vyuo na taasisi za elimu kuhakikisha vinafanya tafiti
kujua mahitaji ya wataalamu wanaotakiwa na kutoa mafunzo yanayoendana na
soko la ajira.
“Nchi
yetu inahitaji kuwa na watalaamu wa fani mbalimbali hivyo ni wajibu wa
vyuo vya elimu ambavyo ndio wazalishaji wa wataalamu hao kuhakikisha
vinatoa wataalamu wenye ujuzi wa kutosha unaoendana na mahitaji ya soko
la ajira ndani na nje ya nchi,” alisema Sefue.
Sefue
alisema kutokana na umuhimu wa takwimu katika maendeleo, Serikali
imekuwa mstari wa mbele kupitia Wizara ya Fedha kuhakikisha inakisaidia
chuo hicho kukabiliana na changamoto zinazokikabili ikiwemo uhaba wa
fedha za kuendeshea chuo hicho.
Aidha,
alisema chuo hicho kuanza kutoa shahada ni hatua kubwa kwasababu chuo
hicho ndio tegemeo la Afrika katika kuzalisha watakwimu wanaosaidia
katika ukusanyaji wa takwimu bora zinazotumika katika kupanga na kupima
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Aidha,
Sefue amekitaka chuo hicho kubuni miradi mbalimbali itakayosaidia
kujipatia fedha kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto zinazojitokeza
chuoni hapo.
Alisema
Chuo Cha Takwimu cha EASTC mwaka huu kimefikisha miaka hamsini ya
utoaji wa mafunzo ya Takwimu na wataalamu mbalimbali wa takwimu
wanaofanya kazi Serikalini wamepitia hapo na hivyo ni wajibu wa Serikali
kuhakikisha inakiendeleza ili kiwe kituo bora zaidi kwa utoaji wa
watakwimu waliobobea.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Professa Innocent Ngalinda amesema chuo
hicho kimejipanga vyema kuhakikisha kinaendelea kuzalisha watakwimu
bora na wenye weledi katika fani ya takwimu.
“Hivi
sasa tumefikia hatua kubwa sana ya kuanza kutoa wahitimu wa Shahada ya
kwanza ya Takwimu Rasmi, tutaendelea kuwa mhimili wa uzalishaji wa
wataalamu hawa muhimu katika maendeleo ya nchi yetu na bara la Afrika
kwa ujumla,” alisema Professa Ngalinda.
Professa
Ngalinda alisema chuo hicho kitaendelea kufanya kazi kwa karibu na nchi
wanachama ili kuhakikisha wahitimu wake wanakuwa chachu ya maendeleo
kwa kusaidia ukusanyaji wa takwimu bora na kwa wakati ili zitumike
katika kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.
Jumla
ya wanafunzi 29 wamehitimu na kutunukiwa Shahada ya kwanza ya Takwimu
Rasmi katika mahafali hayo ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika.
No comments:
Post a Comment