JS76579997Vikosi vya uokoaji wakiendelea na kutoa huduma wakati wa tukio hilo usiku wa kuamkia leoo katika jiji la Paris, nchini Ufaransa.

 

[PARIS] Watu zaidi ya 120 wameuwa na watu wanaodhaniwa kuwa magaidi baada ya kuvamia jiji la Paris, Ufaransa nje ya uwanja wa uliokuwa ukichezwa mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani (Stade de France).
Ripoti zinasema wakati mchezo huo ukiendelea ilisikika milio ya mabomu matatu (3)  yakilia nje ya uwanja huo na kuanza kuwapa hofu mashabiki waliokuwepo uwanjani humo na hata baada ya mechi kumalizika walizuiliwa kutoka nje ya uwanja.
Baada ya kusikika kwa bomu la kwanza rais wa nchi hiyo, Francois Hollande aliondoka uwanjani na kuamuru mipaka ya nchi hiyo ifungwe na safari zote za nje ya nchi sizimamishwe.
Baada ya kuondoka kwa kiongozi huyo inasemekana helikopta zilikuwa zikizunguka uwanja huo unaoingiza watu 80,000.
Inasemekana kuwa wavamiaji hao wamevamia migahawa na bar zilizo nje ya uwanja huo.
Licha ya kuwepo kwa zaidi ya watu 120 wameopoteza maisha inasemekana kuna majeruhi zaidi ya 200 na kuna majeruhi 80 wapo katika hali mbaya.
Rais Oboma tayari ametoa pole kwa uvamizi huo na kuwataka maafisa wa usalama nchini Ufaransa kuchukua hatua za haraka kupambana na watu hao.
Nae waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau amesema ameshtushwa na tukio hilo na kuwapa pole Ufaransa na kuwataka kuchukua hatua kupambana na magaidi hao ili kukomesha vitendo hivyo.
Hata hivyo tayari inasemekana tayari wavamizi 8 wameshauwawa na polisi wa Ufaransa.
Akizungumzia tukio hilo, kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Löw amesema limekuwa tukio la kushtukiza na kuwatoa mchezoni.
Amesema wakati wa pumziko walikuwa kwenye vyumba wakijadili kipi kimetokea na walikuwa waoga wakijiuliza hatima yao itakuwaje.
“Imetuogopesha sana wakati tukiwa kwenye vyumba tulikuwa tukijiuliza kipi kimetokea hivyo hatukuwa tena na mawazo ya mchezo huo akili zetu zilikuwa nini kimetokea,” amesema Löw.
Mchezo huo umemalizika kwa Ufaransa ikishinda goli 2 kwa bila magoli yalifungwa na Adrew Pierre Gignic na Oliver Giroud
Hollande
Rais wa Ufaransa,Francois Hollande akiwa uwanjani hapo wakati wa tukio hilo na maafisa wake wa nchi.
Paris-shooting (4)
Hali ilivyokuwa uwanjani wakati wa tukio hilo.
Paris-shooting (3)
heka heka hiyo uwanjani..
Paris-shooting (2)
watu wakiondoka uwanjani hapo.