Uganda Vs Togo na matokeo ya mechi nyingine za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 (+Video) - LEKULE

Breaking

16 Nov 2015

Uganda Vs Togo na matokeo ya mechi nyingine za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 (+Video)



Ikiwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars bado ina mtihani mgumu wa kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya Algeria baada ya mchezo wa waliocheza uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kukubali kutoa sare ya goli 2-2, kwa upande wa majirani zao timu ya taifa ya Uganda imeendeleza ubabe dhidi ya Togo.
9f9ded05940b18280845b27cf435242b_L
Uganda ambao walikuwa na nafasi nzuri baada ya kuifunga Togo goli 1-0 ugenini iliendeleza ubabe wake mbele ya Togo kwa mara ya pili mfululizo, mchezo wa pili uliochezwa leo November 15 Uganda wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0 hivyo Togo imeaga rasmi harakati za kuendelea kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi.
b41060ebc8ad67513ee96094b9c7eb88_L
Kwa upande wa Uganda bado Farouk Miya aliendelea kuwa mwiba mkali kwa Togo baada ya kuwafunga tena katika mchezo wa marudiano Farouk Miya alifunga goli mbili dakika ya 41 na 45 baada ya Geoffrey Massa kuifungia Uganda goli la kwanza dakika ya 4 ya mchezo, ila mchezo wa November 15 Hamisi Kiiza wa Simba alikuwa benchi kwa dakika zote 90 pamoja na beki wa Yanga anayeichezea Togo Vincent Bossou huku Juuko Murshid wa Simba akicheza kwa dakika zote 90.
Video ya magoli ya Uganda Vs Togo


Matokeo ya mechi nyingine iliyochezwa na kumalizika November 15
  • Zambia 2 – 0 Sudan
Magoli ya Zambia yamefungwa na Lubambo Musonda dakika ya 59 na Winston Kalengo dakika 81

No comments: