SHAMBULIZI LA PARIS: Polisi wasema kuna mshambuliaji mmoja wa tukio hilo alitaka kuingia uwanjani! - LEKULE

Breaking

15 Nov 2015

SHAMBULIZI LA PARIS: Polisi wasema kuna mshambuliaji mmoja wa tukio hilo alitaka kuingia uwanjani!


Paris-shooting (5)
Wanahabarina mashabiki wa soka wakiwa wamejikusanya ndani ya uwanja huo wa mpira ambao nje kulitokea mlipuko huo wa mabomu uliouwa watu zaidi ya 120 usiku wa Novemba 13.2015 katika jiji la Paris.

Na Rabi Hume na mashirika ya habari
Polisi waliokuwa wakikagua mashabiki wa mpira waliokuwa wakiingia uwanjani katika mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani wameuambia mtandao wa Wall Street Journal kuwa kuna mshambuliaji wa tukio hilo alitaka kuingia uwanjani.
Polisi wamesema kuwa mshambulizi huyo alikuwa na tiketi na alitaka kuingia dakika 15 baada ya mchezo kuanza lakini walimgundua wakati wakimkagua na alipofahamu kuwa wamemgundua alikimbia huku akijaribu kulipia mlipuko wake bila mafanikio.
Polisi hao wameongeza kuwa mshambulizi alitaka kuingia ndani ya uwanja ili akafanye shambulizi ndani ya uwanja lakini wakawa wamefanikiwa kulizua tukio hilo.
Baada ya kumdhibiti mshambulizi huyo ulisikika mlipuko wa pili nje ya uwanja huo wa taifa (stade de France) kabla ya mlipuko wa tatu uliosikika karibu na eneo la McDonald.
Akizungumzia tukio hilo mshindi wa 2008 wa mchezo kuruka kwa umbali mrefu kwa watu wenye ulemavu wa miguu, Arnaud Assoumani alikiambia kituo cha Tv cha L’Equipe kuwa baada ya milipuko hiyo hawakuwa na furaha tena ndani ya kiwanja na kila mmoja alikuwa na hofu juu ya maisha yake.
“Tulihisi kuteseka ndani ya uwanja na kila taarifa iliyokuwa ikitujia ilikuwa ya kutisha zaidi,” alisema Assoumani na kuongeza kuwa “Baadae tukapata tangazo kuwa wamefungua mlango na tunaweza kutoka niliona watu wakijaribu kutoka kwa haraka hata kujigonga mlangoni ili waweze kutoka ila ninaamini hawakuumia”
Nchi ya Ufaransa inatarajiwa kuandaa mashindano ya Ulaya mwaka 2016 ambapo michezo 51 itachezwa katika viwanja 10 huku mchezo wa ufunguzi ukifanyika katika uwanja wa Stade de France hapo Julai 10.2016 na kuja kutumika tena kwa fainali mwezi mmoja baadae.
 JS76583353
Vikosi vya usalama wakiwa wamemweka chini ya ulinzi mmoja wa watu waliokutwa eneo ambalo ni hatua chache mmilipuko huo wa mabaomu ulitokea usiku huo wa Novemba 13.2015.

No comments: