Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo,
akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi, wakati wa mkutano wa
Kujitambulisha na kufahamiana na Watendaji wakuu na Maafisa wa Jeshi la
Polisi uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Katika hotuba yake, Mngodo alilipongeza jeshi hilo kwa kusimamia
Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Inspekta
Jenerali wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto)
akiwaongoza watendaji wakuu na maafisa wa jeshi hilo kuimba wimbo wa
maadili wa jeshi hilo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wapili kushoto). Ziara hiyo
iliyofanyika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo, ilikuwa
na lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji hao. Watatu
kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki, wapili kulia ni
Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve, na
kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna
Suleiman Kova.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo,
akizungumza na Watendaji wakuu na Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini
wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam
leo kwa lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji hao. Kushoto
meza kuu ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest
Mangu, Watatu kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki, wapili
kulia ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa jeshi hilo, Clodwig Mtweve,
na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna
Suleiman Kova.
Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akitoa
taarifa ya Jeshi hilo wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi
hilo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha na kufahamiana
na watendaji wa jeshi hilo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia),
akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna
Suleiman Kova baada ya kumaliza ziara yake katika Makao Makuu ya jeshi
hilo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa
jeshi hilo, Clodwig Mtweve, wapili kushoto ni Kamishna wa Polisi Jamii
nchini, Musa Ali Musa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa
ya Jinai, Diwani Athumani.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo ( watano
kulia), Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu
(watano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wakuu na
Maafisa wa jeshi hilo muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea
Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment