15 Nov 2015

Mtaalamu wa Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu kutoka Hospitali za Apollo kuendesha huduma Dar

A 1
Dr Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka hospitali ya Apollo akitoa huduma kwa mtoto Zulea akiwa na mama yake Shamila Idd katika kliniki iliyofanyika siku tatu.’
Na Mwandishi Wetu
Tanzania ni moja ya nchi ambazo ina uhaba mkubwa wa madaktari bingwa wa mfumo wa fahamu
kitendo kinachopelekea nchi kupoteza fedha nyingi kwa kuwapeleka wagonjwa wa
matatizo ya aina hiyo nje ya nchi kupata matibabu na ushauri.
Inakadiriwa kuwa watoto wachanga 1000 kati 4000 wanaozaliwa na tatizo la mfumo wa fahamu
hupatiwa matibabu huku wengine 3000 wakishindwa kupatiwa matibabu.
Kutokana na hali hiyo, Hospitali ya Apollo ya nchini India imemleta nchini daktari
bingwa wa upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wa fahamu ambaye pia ni Mkuu wa
idara ya upasuaji wa magonjwa ya fahamu katika hospitali hiyo DKT ALOK RANJAN ambaye
atakuwa akitoa
huduma na kuwaona wagonjwa wake aliowafanyia upasuaji siku za
nyuma.
Nao baadhi ya wagonjwa waliofika katika kliniki hiyo inayofanyikia katika hospitali ya
hindu mandal jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuhakikisha kwamba
inasaidia katika gharama za matibabu ya watu wanaosafiri nje ya nchi kufuata
matibabu ya magonjwa mbali mbali.
Wamezitaka pia kampuni za bima ya afya kuhudumia wateja wake katika hospitali za kimataifa
badala ya kujikita katika hospitali za hapa nchini pekee.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari ulofanyika tarehe 12 katika hospitali ya hindumandali Dk. Alok Ranjan kutoka Hospitali
za Apollo amewashauri watanzania kubadilisha mtindo wa maisha ili kuepukana
na magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo. anasema kuwa kwa watu wazima
ugonjwa huu mara nying husababishwa na namna mbovu ya ukaaji ambao hudhuru uti
wa mgongo, trauma, shinikizo la damu, ajali, kisukari, uzito wa kupitiliza na
sababu nyinginezo.

Tanzania kwa sasa inakadiriwa kuwa na madaktari wa mfumo wa fahamu 7 ambao wote kwa sasa i watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Dr Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka hospitali ya Apollo akitoa huduma kwa mtoto Zulea akiwa na mama yake Shamila Idd katika kliniki iliyofanyika siku tatu.’

A 2
Bwana Hafidhi Rashid Waziri, mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo na Dr Alok Ranjan katika hospitali ya Apollo Hyderebad akiongea na waandishi wa habari katika Klinik hiyo.

No comments:

Post a Comment