MAHAFARI YA NANE YA CHUO KIKUU CHA KIISLAMU CHA MOROGORO YAFANA. - LEKULE

Breaking

16 Nov 2015

MAHAFARI YA NANE YA CHUO KIKUU CHA KIISLAMU CHA MOROGORO YAFANA.

CHUO Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM)kimesherehekea miaka kumi (10) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, (2005 - 2015). Maadhimisho hayo yameenda sambamba na mahafari ya Nane kati ya  (2008 - 2015).

Mahafali hayo yalihudhuriwa na Mgeni rasmi,  Profesa Dkt. Fadzil Adam, Mkurugenzi wa Chuo cha Kiislam cha Morogoro na  mtafiti wa chuo kikuu cha Zanzibar (SZA),wa Nchini Malaysia Kuala Teregganu.
Pamoja na kusherekea miaka kumi ya chuo hicho pamoja na mahafari ya nane ya chuo hicho  yalihudhuliwa na Mkuu wa chuo hicho Hajjat Mwantum Mlale, Mkuu wa chuo kikuu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza chuo kikuu cha Kiislam cha Morogoro (MUM), Profesa Hamza Mustafa Njozi, pamoja na Mwenyekiti Baraza la chuo hicho Profesa Bakari Lembariti.

Mahafari yalifanyika katika chuo kikuu cha Kiislam cha Morogoro (MUM) mwishoni mwa wiki Novemba 14 mwaka huu.
CHUO Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM)kimesherehekea miaka kumi (10) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 - 2015, maadhimisho hayo yameenda sambamba na mahafari ya Nane ya chuo hicho,(2008 - 2015).


Msafara wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) walipo wasili katika viwanja vya chuo hicho kwaajili ya Sherehe ya kuadhimisha miaka kumi ya chuo hicho pamoja na Mahafari ya wahitimu wa Kozi mbalimbali katika chuo hicho, mahafari yaliyofanyika Morogoro mwishoni mwa wiki Novemba 14,2015.
Wageni wakiwasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM). 
Mkuu wa kitengo cha masomo ya uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM), Salim Said Ali (aliyesimama) akiwakaribisha wageni katika Mahafari yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) Novemba 14,2015.
Mkuu wa chuo hicho Hajjat Mwantum Mlale akiwa katika Mahafari ya nane ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) ambaye pia ndiye aliyokuwa akiwatunuku katika mahari hayo wanafunzi waliofuzu kozi mbalimbali katika chuo hicho.
Mahafari hayo yalifunguliwa kwa Swala ambapo pichani ni baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wakifungua kwa swala. 
 
 
 
 
 Baadhi ya wanafunzi waliofunzu masomo yao na waliohudhuriwa katika mahafari ya Nane ya chuo cha Kiislam cha Morogoro, (MUM) Novemba 14, 2015.
 Baadhi ya wazazi na walezi waliohudhuria katika mahafari ya nane ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) Mkoani Morogoro Novemba 14,2015.
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) akivaa Kofia mara baada ya kutunukiwa kufunzu masomo yao katika mahafari ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo Novemba 14,2015.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) waliopata zawadi baada ya kufauru kwa kiwango cha First Class katika masomo yao katika mahafari yaliyofanyika chuoni hapo Novemba 14,2015.
 Wageni pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafari ya nane ya chuo hicho kumalizika Novemba 14,2015.
Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo hicho katika mahafari ya nane kumalizika yalifanyika chuoni hapo mkoani morogoro Novemba 14,2015..
 Watalamu wa masuala ya Kompyuta wakiwa katika picha ya pamoja katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).
 Majengo ya mabweni ya wasichana na wafulana yaliyopo katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM)
 Jengo la masomo ya Sayansi katika chuo cha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM). 
Ukumbi wa mikutano kwa nje katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).
Ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) kwa ndani.
 Kituo cha redio pamoja na madarasa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).
 Mwandishi na mwalimu wa somo la redio akitoa maelekezo mara baada ya kutembelewa katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).

 Jengo la uongozi katika  Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).

No comments: