15 Nov 2015

Huyu ndio mchezaji mkubwa aliyempoteza binamu yake katika shambulio la Paris na mwingine kunusurika kumpoteza dada yake

Lass-Diarra
Kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Marseille, Lassana Diarra.

Shambulio limelotokea usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi katika jiji la Paris, Ufaransa wakati mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Ufaransa na Ujerumani umeacha simanzi kwa kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Marseille, Lassana Diarra.
Katika shambulio hilo ambalo linakadiliwa kuua watu zaidi 150 limepelekea Diarra kumpoteza binamu yake, Asta Diakote ambae alikuwa moja kati ya watazamaji waliokuwa katika uwanja wa Stade de France kushuhudia mchezo huo wa kirafiki.
Diarra mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Arsenal na Chelsea ambae katika mchezo huo alicheza kwa dakika 80 alisema kuwa binamu yake huyo alikuwa katika mlango wa G wa uwanja huo.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo kupitia ukurasa wake wa Twitter  aliandika “Baada ya tukio lililotokea jana Paris na Saint – Deris ni huzuni kwa hili nisemalo leo”
“Binafsi nimeathiriwa na shambulizi, binamu yangu Asta Diakite ni mmoja ya watu wameoathiriwa katika tukio la Jana ambalo limewapata zaidi ya Wafaransa 100 wasio na hata, alikuwa mhamasishaji dada mkubwa”
“Kwa pamoja tunatakiwa kulindana, tupendane, tuheshimiane na tuwe watu wa amani. Asanteni kwa msaada na meseji zenu. Tuwe makini na waathirika wapumzike kwa amani,” alisema Diarra.
Nae mchezaji mwenzake Diarra wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Antonie Griezman alitangaza kuwa dada yake alinusurika katika shambulio hilo wakati akiwa katika ukumbi wa Bataclan wakati akishuhudia bendi ya kutoka Marekani ya American Rockband Eagles of Death Metal likitumbuiza.

Baada ya tukio hilo michezo yote nchini Ufaransa imesimamishwa kwa muda na Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) limethibitisha kuwepo kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Wingereza na Ufaransa mchezo utakaochezwa Jumanne katika uwanja wa Wembley London, Wingereza.

No comments:

Post a Comment