Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa pili kutoka kushoto) akishiriki katika uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania Oscar Shelukindo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Alex Nkenyenge na Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.
Meneja
Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa tatu kutoka kushoto)
akishiriki katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza uzinduzi wa
Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za
kilomita 10 kwa walemavu. --- GAPCO, kampuni ya mafuta inayoongoza
Tanzania imetangaza udhamini wake wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016
kilomita 10 kwa walemavu.
Akitangaza udhamini huo jana wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ya
Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi
alisema GAPCO inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa
walemavu. “Tumeshuhudia mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu
tuanze kudhamini mwaka 2011 na pia kufurahia faida wanayopata washiriki
na jamii inayozunguka maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka.
Tunayo furaha kufanya kazi na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa
mashindano haya,” alisema Kakwezi.
“Kama
sehemu ya kusaidia jamii ambayo tunafanya biashara, GAPCO Tanzania
imeamua kusaidia wanariadha ambao ni walemavu kwa kudhamini mbio ambazo
wanashiriki walemavu pekee,” alisema. Alisema udhamini wa GAPCO pia
utahusisha usafiri, malazi na chakula kwa washiriki kutoka Dar es Salaam
na pia zawadi za pesa kwa washindi wa mbio hizo za kilomita 10 ambazo
zinafanyika pamoja na mbio nyingine za Kilimanjaro Marathon.
Kakwezi
aliendelea kusema kuwa Kilimanjaro Marathon limekua tukio kubwa
linalovutia washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania na hivyo
limesaidia sana kutangaza vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro
na pia kuwaongezea kipato wafanyabiashara wa Moshi.”.
No comments:
Post a Comment