Mwenyekiti wa Kamati ya Soko la Samaki la Kimataifa la Feri, Ali Kibwana, akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko
mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani vitendo vya unyanyasaji
wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for
Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili katika masoko hayo.
Kushoto ni Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said akizungumza katika mkutano huo.
Mama Lishe wa soko hilo, Taus Barnabas, akichangia neno katika mkutano huo.
Mama Lishe wa soko hilo, Fatuma Saijali (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Kamanda wa Ulinzi na Mazingira wa Soko hilo, Nurdin Hassan akisisitiza jambo kuhusu wanavyo imarisha ulinzi katika soko hilo.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said akizungumza katika mkutano huo.
Mama Lishe wa soko hilo, Taus Barnabas, akichangia neno katika mkutano huo.
Mama Lishe wa soko hilo, Fatuma Saijali (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Mwezeshaji
wa Sheria katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri, Asha Malenda
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo, wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona
jinsi gani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko
hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya
kupinga ukatili katika masoko yaliyopo Manispaa ya Ilala. Kulia ni Mama
Lishe wa soko hilo, Taus Barnabas na Fatuma Saijali.
Ofisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa EfG, Shaban Rulimbiye (kulia), akizungumzia
kuhusu mradi huo wa miaka mitatu wa Mpe Riziki si Matusi.Kamanda wa Ulinzi na Mazingira wa Soko hilo, Nurdin Hassan akisisitiza jambo kuhusu wanavyo imarisha ulinzi katika soko hilo.
Mwonekano wa sehemu ya soko la Samaki la Feri
ENEO
la Lebanon katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri ambalo lipo
jirani na Ikulu jijini Dar es Salaam limedaiwa kuwa ni hatari kwa
wafanyabiashara wa soko hilo na kuwa linadhohofisha uchumi kutokana na
kukithiri kwa watu wasio rasmi.
Hayo
yamebainishwa na Mwezeshaji wa Sheria wa soko hilo, Asha Malenda wakati
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi
wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani
vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya
Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili
katika masoko hayo.
"Tunachangamoto
kubwa sana katika soko letu la Feri tunayoipata kutoka eneo la Lebanon
lenye mwingiliano wa watu wasio rasmi kutoka nje ya soko ambao ni kama
wamejianzishia soko lao na wamekuwa na maamuzi yao lakini viongozi wa
soko la Feri wanashindwa kuwachukulia hatua hali ambayo inatudhalilisha
sisi wafanyabiashara hasa mama lishe na kuharibu uchumi wa soko letu"
alisema Malenda.
Alisema
wengi wa watu waliopo katika eneo hilo lisilo rasmi wamekuwa wakifanya
biashara kiholela huku wakipika vyakula katika maeneo yanayoweza
kuhatarisha afya ya mlaji wakati katika soko hilo kuna eneo maalumu la
mama lishe na wengi wa watu hao wakienda kula eneo hilo rasmi wamekuwa
hawalipi fedha na wakibanwa kulipa wanadiliki kutoa visu na silaha za
jadi kuwatishia wanaodai.
"Eneo
hilo la Lebanon ni hatari na kinachoshangaza linatizamana na Ikulu
lakini hakuna hatua yoyote ya makusudi inayochukuliwa na viongozi wetu
na linapopelekwa kwa viongozi wa kisiasa wanadai waachwe kwani ndio
wapiga kura wao" alisema Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari
Said.
Said
alisema katika soko hilo kuna changoto nyingi za udhalilishaji wanawake
kwa kushikwa katika maungo yao lakini kupitia EfG wamejitahidi
kupunguza changamoto hizo kwani wasaidizi wa sheria waliopatiwa mafunzo
na shirika hilo wanajitahidi kuupenyeza ujuzi waliopata kuifikishia
jamii ambayo imeanza kuelewa kuhusu vitendo hivyo.
Aliongeza
kuwa uvaaji wa nguo za kubana na kuacha vifua wazi kwa upande wa
wanawake pia ulikuwa ukichochea kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji
uliokuwa ukifanywa na vijana wasio rasmi katika eneo hilo la Feri ambao
hawana makazi na maisha yao yapo Feri lakini baada ya kufikiwa na
mafunzo ya EfG hali hiyo imepungua kwa asilimia 80.
Mwezeshaji
Fatuma Saijali alisema changamoto kubwa iliyopo hivi sasa katika soko
hilo ni kuzuiliwa kupika chakula katika eneo hilo la Feri lakini wakati
huo huo kuna kundi la wanawake wamekuwa wakiingiza chakula kutoka
majumbano kwao na kukiuza hivyo kuharibu soko lao la chakula.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Soko hilo, Ali Kibwana alisema mafunzo waliyopata kupitia
EfG yamesaidia sana kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika
soko hilo na kila mtu anayebainika kujihusisha na vitendo hivyo amekuwa
akiitwa na kukanywa na kama akiendelea kuwa mkaidi anachukuliwa hatua
nyingine kwa kufuata kanuni na sheria.
Kamanda
wa Ulinzi na Mazingira wa Soko hilo, Nurdin Hassan amesema hali katika
soko hilo ni nzuri kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na EfG ya kufanya
semina na matamasha ya uhamasishaji hivyo kuifanyajamii kuelewa kuhusu
vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.
Ofisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa EfG, Shaban Rulimbiye alisema Shirika hilo
linaendesha mradi wa miaka mitatu wa Mpe Riziki si Matusi wenye lengo la
kutoa elimu ya kupinga ukatili wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na
udhalilishaji na nia zaidi mradi huo ni kuusambaza hadi katika maeneo
mengine ya nchi.
No comments:
Post a Comment