Mkazi wa Dar es Salaam, Dunia Salumu maarufu kwa jina la Dk. Manyaunyau, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kulipa fidia ya Sh milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha Sh milioni 29.6 kwa njia ya udanganyifu.
Manyaunyau
anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mlalamikaji, Tekra
Modesta kama malipo ya kazi ya kumfufua marehemu kaka yake aliyefahamika
kwa jina moja la Modest ambaye alifariki dunia miaka kadhaa iliyopita.
Akitoa
hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es
Salaam, Flora Haule, alisema mtuhumiwa huyo ametiwa hatiani baada ya
ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka kujitosheleza.
“Mahakama
inatoa hukumu kwa mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na
kulipa fidia ya Sh milioni 10 baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake
ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo,” alisema Hakimu Flora.
Upande
wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne ambao wote waliithibitishia
mahakama juu ya mtuhumiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kwa njia za
udanganyifu.
Awali
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Estar Kyala, aliiambia mahakama kuwa
hakuna kumbukumbu za makosa ya nyuma dhidi ya mshtakiwa na hivyo kuiomba
kutoa adhabu kali ili kuwa fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.
Katika
maelezo ya awali, ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alijipatia kiasi hicho cha
fedha kutoka kwa mlalamikaji kama malipo ya tukio la kutaka kumfufua
kaka wa mlalamikaji.
Ilielezwa
kuwa mtuhumiwa alipokea fedha hizo kwa awamu mbili tofauti ambapo awali
Mei 2007 jijini Dar es Salaam alipewa kiasi cha fedha ambacho
hakikufahamika.
Mei
Mosi, mwaka 2008 mtuhumiwa alipokea kiasi kingine cha fedha kama malipo
kwa ajili ya kumalizia kazi yake ya kumfufua marehemu ambaye ni ndugu
wa mlalamikaji jambo ambalo alishindwa kulitekeleza.
Manyaunyau
amejizolea umaarufu mkubwa katika maeneo mengi nchini kwa kile
kinachodaiwa kuwa anao uwezo wa kutibu na kuwafichua wachawi popote
walipo sambamba na staili yake ya kunyonya damu ya paka akiwa katika
shughuli zake za uganga.
Katika
tukio lililovuta wakazi wengi wa Dar es Salaam, Manyaunyau anadaiwa
kumwibua nyoka ambaye alikuwa tishio na kuzusha hofu kubwa kwa wakazi wa
maeneo ya Manzese Midizini ambapo ilidaiwa kuwa alikuwa akiwagonga watu
katika mazingira ya kutatanisha katika njia inayopita kwenye makaburi.
Inaaminika
kuwa baada ya kuitwa, Dk. Manyaunyau aliweza kumuibua nyoka huyo na
kuonekana hadharani tukio lililohisiwa kuwa ni la kimazingara zaidi.
No comments:
Post a Comment