Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba anatarajia kusafirishwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.
Novemba
7, mwaka huu Dk Bisimba alipata ajali ya gari katika barabara ya Ali
Hassan Mwinyi na kuvunjika mshipa wa paja na goti sanjari na kujeruhiwa
kichwa,bega na mgongo.
Akizungumza
jana akiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI)
ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, Dk Bisimba alisema
kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba anatarajiwa kupelekwa nchini humo
na watoto wake kwa matibabu zaidi.
Alisema
safari yake hiyo siyo kwa sababu ya upungufu wa huduma aliyoipata
kutoka MOI bali ni kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi wa mwili
wake.
“Namshukuru
Mungu naendelea vizuri. Tangu nimekuja hapa MOI, nimesikilizwa na
kuhudumiwa vizuri. Watoto wangu wanashugulikia usafiri na siku yoyote
naenda India ,”alisema.
Meneja
Uhusiano MOI, Jumaa Almasi alisema kuwa Dk Bisimba bado anahitaji
uangalizi wa hali ya juu katika kipindi hiki kutokana na kupata majeraha
mengi kwenye mwili wake.
“Hali ya Dk Bisimba imevunja rekodi. Mbali na kumshughulikia sehemu hizo mbili (paja na goti), kutokana na kuwa na kisukari na presha tumeshindwa kulazimisha matibabu ya haraka kwa viungo vyote,” alisema
“Hali ya Dk Bisimba imevunja rekodi. Mbali na kumshughulikia sehemu hizo mbili (paja na goti), kutokana na kuwa na kisukari na presha tumeshindwa kulazimisha matibabu ya haraka kwa viungo vyote,” alisema
No comments:
Post a Comment