Dk.
Adeline l. Kimambo(kulia) kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akitoa
muhutasari wa Madhara ya Tumbaku mbele ya waandishi wa habari pamoja na
wageni waalikwa waliofika kujadili changamoto wanazokabiliwa nazo hasa
wanapokuwa wanatoa huduma kwa jamii kuhusu matumizi ya Tumbaku na
kuwaomba wadau hao kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo
waliyojiwekea.Katikati ni Dk Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya
Jamii (TPHA).
(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii (TPHA),Dk.
Mashombo Mkamba akizungumza jambo wakati wa majadiliano ni kwa namna
gani wanaweza kupunguza matumizi ya Tumbaku katika jamii unayowazunguka
na hata kuwaomba wadau mbalimbali kushirikiana ili kuongeza nguvu katika
mapambano dhidi ya matumizi ya Tumbaku hasa kwa watoto wadogo ambao ni
nguvu kazi ya baadae.
Dk.Tulitweni
Mwinuka kutoka manispaa ya Temeke akieleza changamoto wanazozipata pale
wanapokuwa wanatoa elimu ya matumizi ya Tumbaku na kusisitiza
changamoto kubwa wanayoipata ni wanasiasa kutotoa ushirikiano wa kutosha
kwa kuhofia kupoteza wapiga kura wao wakati wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment