Bomoabomoa ya nyumba na makazi zilizojengwa kinyume cha sheria iliendelea jana katika Wilaya ya Kinondoni, ambapo Kanisa la Anglikana pamoja na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mivumoni zimekumbwa na bomoabomoa hiyo.
Shughuli
hiyo ya ubomoaji ilianza jana saa 12 asubuhi katika eneo la Mbezi
Jogoo, ambapo nyumba 25, makanisa mawili, fremu mbili za biashara na
sehemu ya kuoshea magari zilibomolewa.
Mbali
na kanisa la Aglikana, kanisa jingine ni la Tanzania Assemblies of God
(TAG) lililopo Bunju B, nyumba ya mwanajeshi ambaye amerejea kutoka
kulinda amani Darfur Sudan nayo imebomolewa na kusababisha mke wa
mwanajeshi huyo kuzirai.
Mbezi Jogoo
Bomoabomoa ilifanyika karibu na kiwanda cha Interchick ambapo nyumba moja na eneo la kuoshea magari vilibomolewa.
Aidha
bomoabomoa iliendelea eneo la Basihaya Bunju ambapo nyumba 19
zilibomolewa pamoja na fremu mbili za biashara ya mbao inayomilikiwa na
Ally Khamis.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Basihaya, Kata ya Bunju, Malinus Ndule alisema nyumba hizo
tayari wananchi wake walilipwa fidia ikiwemo viwanja katika eneo la
Mabwepande.
Waumini waangua vilio
Waumini
wa Kanisa la Tanzania Assemmbles of God (TAG) walifika eneo la tukio
wakiwa na Biblia wakiomba na kuangua kilio huku wakisema Mungu ana
mpango nao.
Akizungumzia
tathimini ya ubomoaji huo, Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka
Mkuya alisema shughuli hiyo inaendelea vyema na ametoa wito kwa wananchi
kutoa ushirikiano kwa kuwafichua vigogo waliojenga kinyume na sheria.
No comments:
Post a Comment