13 Nov 2015

BAVICHA Yawataka Wabunge wa UKAWA Kupigania Katiba Mpya



Wabunge wapya kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi  (Ukawa) wanaotarajia kuingia Bungeni wiki ijayo wametakiwa kupigania kupatikana kwa katiba mpya itakayowezesha kupatikana kwa tume huru ya taifa ya uchaguzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya Shinyanga mjini Bw. Samson Ng’wagi amesema kwamba  wabunge wa ukawa waliopata nafasi ya ubunge wanatakiwa  kusimamia upatikanaji wa katiba mpya ambayo  itasaidia kuwa na tume huru ya uchaguzi ili kuondoa hali ya sintofahamu katika chaguzi zijazo kutokana na tathimini ya uchaguzi uliopita.

Ameongeza kuwa  mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa  vijana hawakuridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi kwa madai ya kuwepo  hujuma na vitendo vya rushwa kutawala pamoja na  vyombo vya dola kutumika kukisaidia chama tawala ili kiendelee kubaki madarakani..

Kwa upande wake Katibu wa BAVICHA wilaya ya Shinyanga mjini Zainab Heri ameitaka   Tume ya uchaguzi Zanzibar(ZEC) imtangaze Maalim Seif kuwa ndiye mshindi  wa Urais aliyechaguliwa na wananchi kuliko kufanya vitendo vinavyoashiria kubaka demokrasia.

No comments:

Post a Comment