Uturuki yainyooshea kidole IS - LEKULE

Breaking

13 Oct 2015

Uturuki yainyooshea kidole IS

Picha ya "Dokuz 8 Haber" inayoonyesha jinsi mlipuko ulivyotokea katika umati wa watu waliokua wakiandamana kwa amani, Oktoba 10, 2015 katika mji wa Ankara, Uturuki.
Serikali ya Uturuki imelitaja Jumatatu wiki hii, kundi la Islamic State (IS) kama mtuhumiwa namba 1 wa mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyotokea wiki iliyopita katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara.
Mashambulizi hayo yaliwaua watu wasiopungua 97 na kusababisha mgawanyiko nchini Uturuki huku baadhi ya raia wakipinga serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan.
Siku mbili baada ya mashambulizi mabayayaliyosababisha vifo vya watu wengi nchini Uturuki, Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu pia alithibitisha kuwa, licha ya majonzi na mvutano viliyoibuka, uchaguzi wa haraka wa bunge utafanyika tarehe 1 Novemba vizuri.
" Kama unaangalia jinsi shambulio hilo lilivyotekelezwa, tunatakiwa kuichukulia Daech (neno fupi la Kiarabu linalomaanisha kundi la IS) kama adui wetu namba 1chetu ", Davutoglu amesemakwenye runinga ya NTV.
" Tuna jina la mtu ambaye anatuelekeza kwenye na kundi hilo ", ameongeza Davutoglu.
Jumamosi asubuhi Oktoba 10, watu wawili walijilipua mbele ya kituo kikuu cha treni katika mji mkuu wa Uturuki katikati ya umati wa watu waliokua wameitikia wito wa vyama vya wafanyakazi, mashirika yasio ya kiserikali na vyama vya mrengo wa kushoto na kusababisha watu 97 kuuawa. Wanaharakati hao walikua wakiandamana wakipinga kuanzishwa kwa mapigano kati ya jeshi la Uturuki na waasi wa Kishia wa Huthi.
Ripoti ya mwisho, ambayo bado ni ya muda, iliyochapishwa na viongozi wa Uturuki inaonyesha kuwa watu 97 walifariki na wengine 507 walijeruhiwa, ikiwa ni pamoja na majeruhi 65 ambao wako katika hali mbaya.
Hata kama amelinyooshea kidole kundi la Islamic State, Ahmet Davutoglu , hata hivyo, amewataja waasi wa Kikurdi wa (PKK) au waasi wa DHKP-C, ambao amesema kuwa ni washukiwa wa kubwa wanaoendesha mashambulizi mbalimbali nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki, wachunguzi wanaamini kwamba kifaa kiliyolipuka katika mji wa Ankara ni aina moja na kile kiliyotumiwa katika shambulio la Suruç (Kusini) mwezi Julai.

No comments: