Mwenyekiti wa NLD, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Dkt. Emmanuel Makaidi amefariki leo majira mchana katika hospitali ya Nangao mkoani Lindi.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Dkt. Makaidi ambaye alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Masasi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Dkt. Makaidi ni mgombea ubunge wa tano kufariki katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
LEKULE inatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa Dkt. Emmanuel Makaidi na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment